SIMBA YATOA DOZI NYINGINE ZANZIBAR
‘Wekundu
wa Msimbazi’ Simba wameendelea kushusha vipigo kwenye mechi zao za
kirafiki visiwani Zanzibar baada ya leo kugawa kipigo cha goli 3-0 na
kuilaza timu ya Jang’ombe Boys pambano lililopigwa kwenye dimba la Amaan
visiwani Zanzibar jioni ya leo.
Elius Maguli alianza kuifungia
Simba goli la kwanza dakika ya 12, dakika ya 17 Michael Mgimwa
akaiandikia Simba bao la pili kabla ya Samir Omary kuhitimisha kalamu ya
magoli kwa upande wa Simba kwa kufunga goli la tatu dakika ya 81.
Licha ya ushindi huo wa goli 3-0
kocha wa Simba amelalamikia suala la wachezaji wa Tanzania na Afrika kwa
ujumla kushindwa kufunga pale wanapopata nafasi.
Kwa upande wa kocha wa Jang’ombe
Boys Issa Masha yeye amesema Simba ni timu kubwa na timu yake
imejitahidi japo wamefanya mazoezi kwa muda mfupi na kukutana na Simba
ambayo inamazoezi kwa muda wa miezi miwili.
Simba itahitimisha mchezo wake wa
kirafiki visiwani Zanzibar kwa kucheza na KMKM siku ya Jumatano mchezo
unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:00 usiku kwenye uwanja wa Amaan.
No comments:
Post a Comment