Thiery Henry: “I went to sleep
knowing what to do. I always thought if I don’t move, Abidal won’t,
Iniesta won’t get the ball. It’s constant.”
Hayo Ni maneno ya Thierry Henry
Na Mimi Yamenikosha sana na nimeona ngoja nitie maneno yangu
kuzungumzia kuhusu mpira wa miguu…
Unajua kwa sisi mashabiki wa
mpira tunaishia tu kujua kuhusu formation za team labda sana ukijitahidi
utajua kuhusu filosofi flani ya timu flani basi hapa tumekua
tumeridhika na tuna-enjoy mpira kwa kiasi kile tunachouelewa …
Ila mpira kama mpira una utaalamu
wake ambao watu wengi hua hatuufahamu wala hatujishughulishi kuujua
ambao labda utaalamu huu ungeweza kutubadili mawazo na kutuongezea sana
radha ya soka.
Kitu kinacholeta ladha ya mpira
na utofauti wa timu moja na nyingine sio tu pekee filosofi ya timu na
wala sio tu formation pekee inayotumiwa na timu .. utofauti wa team moja
hadi nyingine unaletwa na jinsi gani utautembeza mpira wenu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine kutumia watu gani na ni kwanini mtu au watu
hao ndio watumike, kumbe basi timu zinaweza kushare formation moja, na
pia zinaweza kushare filosofi moja ya mpira ila bado njia zao za
kupitisha hiyo mipira kutoka eneo moja hadi lingine zikawa tofauti.
Na kutokana na hili suala ndio
maana kuna muda hata zile team kubwa zenye wachezaji wazuri hua
zinafungwa. Kinachowafanya wafungwe hapa sio formation na wala sio
kwakua mchezaji flani anacheza mahali flani ndio maana timu imefungwa
kwakua sio nafasi yake, bali kinachofanya kupoteza mechi ni mbinu za
kupitisha mipira za timu husika ilioshinda.
Ukisikia neno ‘Game Plan’ hua
haliishii tu kwenye formation na filosofi za timu basi, kama ingekua
inaishia hapa basi makocha wenye experience zao au wale high profile
managers wasingekua wanajisumbua kwenda uwanjani kuisoma timu pinzani
ikicheza na timu nyingine kwakua kutokana na experince zao wangeelewa tu
wacheze nazo vipi hizo timu wakikutana nazo kwakua mara nyingi hua
wanajua vitu vingi sana kweye soka.
Na pia mnaweza mkakutana na timu
mbili tofauti mnacheza mpira unaofanana na formation inayofanana ila
bado matokeo yakawa tofauti hii ni kutokana na hamuwezi kufanana njia za
kupitisha mipira wachezaji mnaotumia kuanzisha mashambulizi wapo kwenye
position zipi na pia ni mchezaji gani anaanza kukaba wapi, hadi kufika
wapi mnaanza kungia kwa nguvu kuchukua mpira, mnaiba vipi muda kuvizia
kuanzisha shambulizi hamuwezi kufanana hivi vitu.
Makocha wanakua wana njia nyingi
za kuwaambia wachezaji wao wapitishe mipira kutokana mechi husika pamoja
na uwezo wa wachezaji waliokuwepo uwanjani siku hiyo, hivyo basi kila
mechi hasa hizi mechi muhimu hua zina game plan yake ya tofauti ambayo
hii ni zaidi ya kuona formation uwanjani. Makocha wanaamua kwenda
viwanjani kuangalia mpinzani anavyocheza kwakua huwez kuiona game plan
ya mpinzani wako kwenye TV kwakua TV zinaonesha tu sehemu ambao mpira
ulipo.
Mpira hua unachezwa sehemu mbili
yule anaekua na mpira kwa wakati huo pamoja na wale wasiokua na mpira
ina maana positioning zao ni jinsi gani timu inajipanga kama mpira wanao
wao, ni mchezaji gani hua anakimbia kwenye eneo gani kama team yake
ina mpira hivi ndio vitu ambavyo makocha au scouts wanaenda kuvitazama
uwanjani ambavyo huwezi kuviona kwenye TV, TV itakuonesha mpira ulipo
mara mchezaji kapokea pasi alipotokea huwezi kuona labda hadi replay .
Henry anakwambia alikua anaenda
kulala akijua kua ili Abidal aweze kuachia mpira miguuni mwake lazima
yeye awe amefika eneo fulani na asipofika hilo eneo ina maana Abidal
hawez kuachia mpira hapa ikumbukwe kua mpira huu ambao upo kwa Abidal
hautoki miguuni kwa Abidal moja kwa moja hadi kwa Thierry Henry la hasha
ila unapitia kwa Iniesta ambae nae kwa wakati huo anakua hana mpira
kwakua mpira upo miguuni kwa Abidal.
Mpaka hapa kuna kua kuna watu watatu wanacheza mpira mmoja ambao upo miguuni mwa mtu mmoja tu ambae ni Abidal.
Kama Thiery Henry asipofanya hii
move anaweza kuisababishia timu yake iwe in trouble kwakua anaweza
kufanya Abidal asifanye maamuzi sahihi kama ilivyokua planned, kwaiyo
Henry akifanya move yake na Iniesta yeye kazi yake inakua kumtupia tu
Henry kwakua anajua ni wapi alipo, hapa sasa Iniesta anaweza
akakupumbaza labda kwa kupiga chenga mbili tatu ili akushawishi kua ana
mpa Henry labda tu kwakutaka kuuachia mpira miguuni mwake kwakua
amekabwa kumbe anakua anakudanganya Thierry Henry ndio anakua mtu sahihi
alitaka kumpa.
Hapa ndio mpira hua unachezwa na
ndio maana kwa watu wenye uelewa haachi kwenda kuangalia mpira uwanjani
hata kama unaoneshwa kwenye TV kwakua akienda uwanjani anaona mchezo
mzima ulivyo.
Hizi formation zipo ili tu
wachezaji wakae kwenye system flan ila kinachofanya team ifungwe au
ipate ushindi sio tu formation pekee mpira hua hauishii hapo ni ile game
plan ndio inayosababisha timu kufungwa au kushinda.
Kuna muda unaweza kuona timu ile
ile moja na wachezaji wanajipanga vile vile kwenye mechi kama tano
mfululizo na mechi zote timu hiyo hiyo moja kwa kikosi kile kile inapata
matokeo ya ushindi, kumbe basi hapa wanachokua wanabadilisha ni jinsi
gani ya kucheza, kupitisha ile mipira yao wakati wa kushambulia na style
yao ya kuzuia wakati wa kukaba.
Kwa maana hii basi ni kwamba
hamna timu yeyote duniani hata kama iwe bora kiasi gani inayoweza
kucheza yenyewe tu bila mwalimu wa kuwaelekeza, na ndio maana hata wale
wachezaji magwiji kabisa waliowahi kuwa bora duniani hua na wao wanaenda
kusomea kua walimu wa mpira.
Sisi mashabiki wa mpira tunakua
rahisi mno kusema na kulalamika “mchezaji flani hawez kucheza kama
mchezaji wetu flani, mara me huyu flani anaudhi sana kocha nae kwanini
hamtoi anaendelea tu kumpanga mi naudhika” *** tambua kama hata wewe
umeona flani hawezi kucheza kama flani aliekua benchi basi ujue hata
mwalimu anaewafundisha wachezaji hao amewaona na anawajua kuwa flani
hajui kufanya kitu hiki na isitoshe anakua nao kila siku mazoezini.
Makocha wote duniani wanaangalia
zaidi game plan zao kuliko uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, ndio maana kwa
wanaojua soka wanakwambia kujua mpira na kudumu kwenye mchezo wa mpira
sio kipaji tu unaweza ukawa na kipaji na usifike popote, muhimu ni
kufanya mazoezi kujituma sana na kuwa na nidhamu kweli kweli nje na
ndani ya uwanja na pia kufata maelekezo ya mwalimu hapa utafanikiwa
kimpira.
Ukimkuta mchezaji mwenye kipaji
cha ukweli, na ana nidhamu ya hali ya juu anafanya mazoezi kisawasawa na
kusikiliza walimu wao hawa ndio hua wanafanikiwa mno.
Kwaiyo ushauri wangu kwa watu wa
mpira ni kwamba, tunapoenda kuangalia mpira kabla hujaanza kulalamika
kwanini flani anachezeshwa hivi kwanini flani hachezi na kuanza
kukasirika, jaribu kutafakari kwanza ni nini kocha ana hitaji kutoka
sehemu hiyo, kama ukitafakari na ukaelewa labda inaweza kukusaidia
kuenjoy huo mchezo badala ya kukasirika na itakusaidia pia kuelewa.
Na hata hao wanaokua nje haina
maana watakaa nje forever, kuna wakati inakua wanakua wanamechi zao
watacheza au labda pia walimu wao wanakua wanawatafutia njia ya
kuwaingiza kikosi cha kwanza bila kuharibu muendelezo wa timu.
Naishia hapa namalizia kwakusema
kua nimekoshwa sana na maneno ya Thiery Henry sentensi chache tu ila
zimebeba maana nzima ya football.
No comments:
Post a Comment