HAJIBU, KIIZA, WAIONGOZA SIMBA KUUA MECHI YA TANO MFULULIZO VISIWANI ZANZIBAR
Klabu ya wekundu wa msimbazi
imehitimisha mechi za kirafiki visiwani Zanzibar kwa kushinda mchezo
wake wa leo iliyocheza dhidi ya KMKM kwa kuichapa klabu hiyo goli 3-2
mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar ukiwa ni mchezo wake wa
tano na kufanikiwa kushinda michezo yake yote ya kirafiki iliyocheza
ikiwa visiwani humo.
KMKM ndio walikuwa wakwanza
kufunga magoli yote mawili kupitia kwa mchezaji wao Mateo Antony Simon
akifunga magoli hayo dakika ya 20 na 25 ya mchezo huo lakini Hamisi
Kiiza ‘Diego’ akaipatia Simba goli la kwanza dakika ya 42 kipini cha
kwanza na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku KMKM ikiwa mbele kwa
goli 2-1.
Kipindi cha pili Simba walianza
kwa kasi kubwa na KMKM wakaonekana wakiwa wamechoka na kushindwa
kuendana na kasi ya Simba, ambapo mshambuliaji chipukizi wa Simba
Ibrahih Ajib aliifungia klabu yake mabao mawili ya harakaharaka dakika
ya 75 na 78 akaipa ushindi klabu hiyo wa goli 3-2. Mabao hayo yakiwa
yamechangiwa na kiungo Mwinyi Kazimoto na kiungo aliyesajiliwa kutoka
Zimbabwe Jastice Majiva.
Kesho Simba inatarajiwa kurejea
jijini Dar es Salaam ambapo ilicheza mechi tano za kirafiki ikiwa
visiwani Zanzibar. Mcheo wa kwanza Simba ilishinda kwa goli 2-1 dhidi ya
Kombaini ya Zanzibar, mechi ya pili Simba ikashinda kwa goli 4-0
wakati mchezo wa tatu ilicheza dhidi ya Polisi ya Zanzibar na kushinda
kwa goli 2-0 huku mchezo wake wa nne ikishinda pia kwa goli 3-0 mbele ya
Jang’ombe na kumaliza na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya KMKM.
No comments:
Post a Comment