SELEMANI Matola |
WASHABIKI wa klabu ya soka
bila shaka walikuwa na maswali mengi pindi alipoondoka Ramadhani Singano
'Messi' na kuna baadhi walikuwa na shaka na pengo lake, lakini
njoo uangalie vita ya namba ya nafasi ya winga, ndipo
utakapokubali kuwa, Simba ina 'warithi' kibao, hivyo pengo hilo kwa sasa
hakuna.
Lakini, hili tisa, Kocha msaidizi
wa Simba, Selemani Matola amesema, pamoja na ushindani huo, lakini
kuna kijana mmoja matata ambaye anaitendea haki nafasi ambayo Singano alikuwa
anacheza, huyu ni Peter Mwalyanzi.
Matola ambaye ndiye kocha
aliyewaibua wachezaji wengi vijana akiwemo Ramadhani Singano, alimweleza
mwandishi wa habari hizi akiwa katika mazoezi ya jana (juzi)
yanayoendelea jijin kuwa, Mwalyanzi ni kati ya wachezaji wanaoweza
kucheza namba zote za winga, lakini ana kiwango cha kuaminika katika
kikosi cha msimu huu.
Kocha huyo alisema, ujio wa
Peter Mwalyanzi, Hamis Kiiza, Simon Sserunkuma na Mussa Hassan Mgosi
umeziba kabisa pengo la Messi, na kukiri kuwa, ushindani
wa idara ya ushambuliaji wa pembeni utakuwa mkubwa na kuliweka
katika wakati mgumu benchi la ufundi.
Alisema, tangu Simba ilipanza
kambi ya majuma mawili mjini Lushoto amebaini ugumu wa nani apangwe na yupi wa
kusubiri kati ya Mwalyanzi (Peter) Hamis Kiiza, Simon Sserunkuma na Mgosi
ambao wote wanamudu kucheza kama winga.
Aliongeza kuwa, licha ya
ushindani uliopo, wachezaji wote hao ni mafundi wa kucheza
zaidi ya nafasi mbili uwanjani, hatua ambayo inawapa makocha ugumu wa kupanga
kikosi cha kwanza.
"Mwalyanzi ana uwezo mkubwa wa
kucheza kama winga wa kushoto, lakini ni fundi pia akipangwa kama kiungo
mshambuliaji".
"Kiiza (Hamis) Mgosi na Simon
(Sserunkuma) nao wapo katika kiwango kizuri kucheza kama winga na hata
washambuliaji, hapo ndipo unapoona kazi ya kupanga kikosi itakavyokuwa ngumu
zaidi msimu huu" alisema Matola.
Matola alisema, mfumo wa
sasa wa kocha Dylan Kerr unamtaka kila mchezaji kuwa na uwezo wa kucheza
katika nafasi mbili na kwamba kila mchezaji wa kikosi cha msimu ujao
anamudu vigezo na masharti.
Katika mazozi ya kila
siku yanayoendelea visiwani hapa (Unguja) kocha Kerr amekuwa
akiwapanga wachezaji katika idara tofauti na kila mmoja alionesha kumudu
kwenda na mfumo autakao mzungu huyu.
No comments:
Post a Comment