Tuesday, August 4, 2015

MAGUFULI ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR LEO,VIFIJO NA NDEREMO VYATAWALA  

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
 Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015. 
Picha ya pamoja
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar.
Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
 Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa Lumumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
 Shamra shamra na vigele vigele vya wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM vikiwa vimetawala nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu  ya CCM mtaa wa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo
 Gari ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Jonh Pombe Magufuli pamoja na Mgombea mwenza Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa tayari kwa ajili ya kuwapeleka kuchukua fomu za kuwania Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 
Mgombea Mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi akiwapungia mkono wananchi na wafuasi wa chama hicho nje ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu  ya CCM mtaa wa Lumumba wakishangilia wakati Mgombea alipokuwa ikielekea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
 Dkt Magufuli akiwapungia baadhi ya Wanachi hawapo pichani alipokuwa akiwasili ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi akiwa ameambatana na Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini
Dkt John Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama cha CCM,katka Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
 Ilikuwa ni shangwe pia nje ya ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Wananchi wakirekodi msafara wa Dkt Magufuli 

Baadhi ya Wananchi wakichukua matukio kwa simu.

No comments:

Post a Comment