Thursday, August 6, 2015

BREAKING NEWS!!!

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AJIUZULU NYAZIFA ZOTE CUF NA UKAWA, ABAKI MWANACHAMA WA KAWAIDA

????????????????????????????????????
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock leo jijini Dar es salaam wakati akitangaza kujuuzulu nyazifa zake zote katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kutokana kile alichokiita dhamira inamsuta.

????????????????????????????????????
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akionyesha rasimu ya katiba iliyoandaliwa na tume ya katiba mpya iliyokuwa ikipendekezwa  iliyoandaliwa na Jaji Joseph Warioba ambayo anadai imefinyangwa.
……………………………………………………………………………..
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama hicho akisema  dhamira inamsuta. 
Profesa Ibrahim Lipumba Amezungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo, Profesa Lipumba amesema  amejitahidi kujenga chama hicho hasa Tanzania bara, amejenga umoja wa Wazanzibari hivyo anajiuzulu kulinda heshima yake.
Amesema ameikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu, barua yake ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yake imelipiwa mpaka mwaka 2020.
Ameeleza sababu  za kujiuzulu ni Umoja wa huo wa UKAWA kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la katiba.
Profesa Lipumba amekiri kushiriki katika vikao mbalimbali vya Ukawa mpaka hapa walipofikia . lakini akasema . Nafsi yangu inanisuta kuwa katika maamuzi yetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa za utu, uadilifu, uzalendo, uwajibikaji,, umoja,na uwazi .

No comments:

Post a Comment