Saturday, August 8, 2015

FLOYD MAYWEATHER AJITETEA KWA KUMCHAGUA KIBONDE

2B297AD500000578-3187536-image-a-34_1438907110298
Floyd Mayweather amewambia watu waanze kununua ticket za ndege kabisa na kuweka oda ya vyumba vya hotel huko Las Vegas kuja kuangalia pambano lake la mwisho mwezi September mwaka huu.
Watu wengi walitegemea kwamba Mayweather angepambana na Amir Khan lakini hajawa hivyo. Kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema kwamba Amir Khan hayupo tayari kumbana na yeye. Anatakia Khan ampige bondia Danny Garcia kwanza ndio atakua amefuzu kiwango cha kucheza na yeye.
Pia amemaliza kabisa uwezekano wa yeye kupigana na Khan kwani amesema hata kwenye pambano hili akipigwa hana mpango wa kuongeza pambano lingine. Ametosheka na mapambano 49 aliyocheza kwenye career yake ya ngumi.
Licha ya kujitetea kote lakini bado watu wanalaumu uchaguzi wa Andre Berto badala ya Amir Khan ambapo lingekua pambano lingine lenye mvuto mkubwa.

No comments:

Post a Comment