Wednesday, August 12, 2015

HII NI TAARIFA RASMI KUTOKA SIMBA SC

Awadh Juma (kushoto) akishangilia pamoja na  Hamis Kiiza (katikati) na
SIMBA SPORTS CLUB
Dar es salaam
TAARIFA KWA VYOMBO VYA VYA HABARI
Klabu ya Simba inayo furaha kuwafahamisha wapenzi wa mpira wa miguu, hususani wanachama na wapenzi wake kuwa tarehe 15-8-2015, siku ya Jumamosi itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya klabu ya URA ya nchini Uganda
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa taifa uliopo jijini Dar es salaam.
Pia klabu ya Simba inawaarifu kuwa mazoezi ya timu yake yataendelea tena kesho jioni baada ya kuwapa mapumziko mafupi wachezaji wake
Mazoezi hayo yanatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Polisi Kilwa road.
Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba
Simba nguvu moja

No comments:

Post a Comment