Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini
(TRA) Ijumaa ya Agosti 14 inatarajia kuendesha semina ya kodi kwa
viongozi wa klabu zilizopo jijini Dar es salaam katika hoteli ya Tiffany
iliyopo eneo la Kisutu.
TRA itaendesha semina hiyo kwa
klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo
viongozi wakuu wa klabu hizo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu
wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.
Kwa kuanzia TRA itaendesha semina
hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa klabu
zilizopo mikoani kwa lengo la viongozi wa klabu kutambua umuhimu wa
ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.
Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi
mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la
Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi
daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam
mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.
No comments:
Post a Comment