Thursday, August 13, 2015

MREMBO HUYU AFARIKI BAADA YA KUBUGIA DAWA ZA KUPUNGUZA UNENE,ALIZINUNUA KWENYE MTANDAO!!


Ni binti mrembo wa miaka 21 aliyefikia Chuoni kimasomo ambapo alichukua maamuzi ya kununua dawa za kupunguza/kujikinga na unene alizozinunua kwenye mtandao (online).
April 12 2015 ndio ilikua siku yake ya mwisho duniani baada ya kulazwa hospitali na chanzo cha kifo chake kikiaminika ni hivyo vidonge ambavyo inasemekana vilikua na sumuMama yake mzazi ameongea na kusema Madaktari wasingeweza

kuokoa maisha yake, kunywa hizo dawa ni sawa na kujisogeza karibu na kifo, zinasababisha pia mwili upate joto kupitiliza na kusababisha pia ini kushindwa kufanya kazi.

Eloise alipoanza kuona hali iko tofauti baada ya kunywa dawa alikwenda hospitali mwenyewe lakini ikawa imeshaharibu tayari, alichelewa kwenda.
Haikufahamika ni vidonge vingapi alimeza na alivitumia kwa muda gani lakini Polisi wa Uingereza wametoa onyo kwa yeyote mwenye mpango wa kununua dawa online aachane nao tena sanasana kupitia websites ambazo hazijasajiliwa.

No comments:

Post a Comment