Mlinda
mlango mkongwe nchini Juma Kaseja amesema kumekuwa na timu nyingi
ambazo zimekuwa zikitaka kumsajili baada ya kupata ruhusa rasmi kutoka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujiunga na timu yoyote
itakayokuwa inahitaji huduma yake wakati akisubiri hatma ya kesi yake na
klabu ya Yanga.
Golikipa huyo wa zamani wa timu
ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amevitaja baadhi ya vilabu ambavyo
vimekuwa vikiiwinda saini yake kuwa ni Mbeya City, Ndanda FC pamoja na
African Sports.
Habari za ndani zaidi zinasema
kuwa, Kaseja tarari ameshamalizana na Coastal Union ya Tanga na amerejea
jijini Dar es Salaam kuja kuchukua vitu vyake tayari kwa kuanza maisha
mapya kwenye klabu ya ‘Wagosi wa Kaya’ kwa ajili ya msimu ujao.
Hapa chini unapata fursa ya
kumsikiliza Kaseja akivitaja baadhi a vilabu vinavyopigana vikumbo
kumsajili, bofya hapo kusikiliza stori kamili.
No comments:
Post a Comment