Saturday, August 22, 2015

Kilichotokea kwa Pedro Man Utd, hawa ni wachezaji 11 waliodakwa dakika za mwisho na timu pinzani



Baada ya dili la Pedro kusajiliwa na Manchester kuharibiwa na Chelsea, imefanya nikumbuke jinsi gani hiki kitendo kuwa ni cha kawaida sana kwenye harakati za usajili hasa muda wa mwishoni kama huu. Lakini kwa ujumla Manchester wameonekana kuwa vibonde sana kwenye michezo hii ya kupokonywa tonge mdomoni. Hii ni list ya wachezaji ambao walisajili na timu tofuati katika harakati za kujiunga na timu nyingine.
Robinho
Chelsea walishaanza kuuza jezi za Robinho zikiwa na jina lake nyuma lakini michezo ikachezwa mara jamaa huyo kadondoka Manchester City akitokea Real Madrid.
Emmanuel Petit
Tottenham walishalipa kiasi kidogo kwa ajili ya kodi ya Petit ili ajiunge na Spurs. Lakini kama kawa wakali wa michezo yao nyuma ya pazia wasababisha jamaa atoke Monaco na kuhamia Arsenal badala ya Spurs.
Ronaldinho
Jamaa anasema ilikua ni masaa 48 kabla sijasaini mkataba na Manchester nikiwa ndani ya jiji lao kabisa ndipo Barcelona wakaja na dili la maana na kunichukua.
Roy Keane
Huyu jamaa alishakubaliana kila kitu kuhamia Blackburn Rovers na mambo yote yapo sawa, lakini dakika za mwisho akapokea simu kutoka kwa Sir Alex Ferguson na mambo yote yakabadilika.
Mohamed Salah
Liverpool walifanya nae mazungumzo kwa muda wa miezi miwili. Lakini tatizo lao la kutokufanya maamuzi Chelsea wamsajili fasta.
Lucas Moura
Manchester united walikua wanakamilisha mpango mzima na kumsajili mchezaji huyu lakini PSG wakaja na offa kubwa kupita kiasi ukifananisha na waliyotoa Man united na kubadilisha upepo wote.
Park Chu Young
Ilibidi aanze safari ya kwenda Lile kwa ajili ya vipimo vya afya lakini safari ile ilibadilirika na kumfanya aende London kujiunga na Arsenal dakika za mwisho.
John Obi Mikel
Huyu jamaa alishavaa hadi jezi ya Manchester lakini Chelsea wakaja mbele na kuwapiku na kumfanya kuwa mchezaji wao halali akitoka FC Lyn Oslo.
Willian
Huyu jamaa alikubaliana dili na alifanya hadi vipimo vya afya na Spurs kabla hajabadili mawazo yake ambayo yaliwashtua wengi na kuhamia Chelsea.
Aaron Ramsey
Manchester united wasema kupitia website yao official kwamba dau lao limeshakubaliwa na Cardiff na huyu jamaa atajiunga nao hivi karibuni. Wakaja Arsenal na watu wao kwa mbele na kumchukua Ramsey.

No comments:

Post a Comment