Thursday, August 20, 2015

WENGER AMKATAA MCHEZAJI WA SEVILLA

gun__1408094185_wenger_pressconf_150814_1
Arsene Wenger mmoja kati ya makocha ambaye hapendwi sana na mashabiki wake kutokana na tabia yake ya kusajili kwa style tofauti sana na club nyingine. Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza, Wenger bado ana imani kubwa na wachezaji wake.
Kwenye moja ya majibu aliyoyatoa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mechi iliyopita Wenger alisema, “Tunafanya kazi kwa bidii sana, tume-focus kuimarisha kikosi chetu tulichonacho. Ukipoteza mchezo unapata mawazo au hamu ya kusajili wachezaji wapya hasa kwa kipindi hiki. Lakini tungeweza kushinda ule mchezo bila ya kubadilisha kikosi kilichopo.”
Pia Wenger aliulizwa kuhusu tetesi nyingine ya team yake kutaka kumsajili mchezaji Grzegorz Krychowiak kutoka Sevilla. Bila kupindisha manager Wenger alijibu straight “No”. Kwa hiyo mchezaji huyo wa Sevilla kuanzia sasa ametoka kwenye list ya tetesi za kuelekea Arsenal.

No comments:

Post a Comment