Mwanariadha wa
Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika
mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt
alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake
medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi
zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.
Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na
Gatlin alitumia sekunde 19.74.
Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa Bahamas akiridhika na medali ya fedha.
Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99.
Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada, Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mchujo.
Hata hivyo Sum, alinusurika pale muda wake wa dakika 1.57.56 ulikuwa wa kasi zaidi kati ya wale waliomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao, na hivyo kufuzu kwa fainali.
No comments:
Post a Comment