Thursday, August 13, 2015

LUIS NANI NA VAN PERSIE WAPO HATARINI KUSHAMBULIWA NA MAGAIDI BAADA YA TUKIO HILI

Robin-van-Persie-Fenerbahce1111_2015070709241568
Robin Van Persie na Luis Nani hivi sasa ni wachezaji halali wa club ya Fenerbahce ya uturuki. Wote wawili wametokea club ya Manchester united na kujiunga na wababe hao wa uturuki.
Kutokana na tukio la pili la mashambulizi ya kighaidi dhidi ya wachezaji wa Fenerbahce limeleta wasiwasi mkubwa kwa nyota hawa wawili. Hivi sasa mchezaji Mehmet Topal ameshambuliwa kwa risasi na waliotajwa kuwa ni maghaidi. Shukrani kwa gari lake la gharama Mercedez G Class ambalo kiyoo chake ni bullet proof kwa hiyo risasi haikumfikia. Lakini kama angekua anaendesha gari la kawaida basi hivi sasa yangekua mengine.
2B4679CC00000578-3193804-image-a-34_1439303494867
Hii ni mara ya pili kwa Fenerbahce kushambuliwa na wanaotajwa kuwa ni maghaidi. Mara ya kwanza ilikua ni April 4 ambapo club hiyo ilikua inaendea kwenye mechi ya ligi dhidi ya Caykur Rizespor.
2B4620FC00000578-0-image-a-32_1439302385902
Kwasababu target ya watu hao ni club ya Fernebache na wachezaji wake. Robin Van Persie na Nani wapo kwenye wasiwasi mkubwa kwasababu ni mastaa wa club hiyo.

No comments:

Post a Comment