Baada ya
wiki ngumu Stamford Bridge, Chelsea wakianza vibaya huku pia Jose Mourinho
akimuondoa katika benchi, daktari Eva Carneiro kwa madai ya kupoteza muda kwa
kumtibia Eden Hazard, sasa Ex-boyfriend wa daktari huyo amefunguka na kusema
yaliyojiri.
Mpenzi huyo
wa zamani wa Eva, aitwaye Rupert Patterson-ward amesema aliachana na Eva kwa
sababu alimwambia alikua akitembea na mchezaji mmoja klabuni hapo.
Rupert
aliyekutana na Eva 2011 kabla hawaja achana 2013 anasema kwamba Eva ni mtu wa
mapenzi sana na kwamba anapenda zaidi ngono.
Rupert
anadai walitaka kufanya familia na kuoana lakini Eva alimfukuza na kumwambia
kuwa alilala na mchezaji mmoja kikosini hapo.
Hata hivyo
habari hizi hazina mahusiano ya moja kwa moja na kitendo cha Mourinho kumfukuza
katika benchi mwanadada huyo.
Gazeti la
Manchester Evening wiki hii liliripoti kuwa huenda Ivanovic akawekwa benchi
kutokana na kuchukizwa na maamuzi ya Mourinho kumfukuza daktari huyo mrembo.
Hata hivyo
wakitoa maoni wasomaji wa gazeti hilo, wamesema kila mtu ana haki ya kufanya
mapenzi huku wakiamini inaweza pia kuwa mbinu za kumchafua Eva zinazofanywa na
mpenzi wake huyo wa zamani.
No comments:
Post a Comment