Thursday, August 13, 2015

Mourinho amtimua daktari wa timu




Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anapaswa kuomba msamaha kwa daktari wa timu Eva Carneiro ''kwa kumfedhehesha hadharani'' daktari wa zamani wa Liverpool amesema.
Peter Brukner ambaye kwa sasa ni ni daktari wa timu ya krikteti ya Australia amesema Mourinho hakuwa sahihi kwa aslilimia mia moja na Carneiro hakuwa na jukumu tofauti na la siku zote.Carneiro mwenye umri wa miaka 41 alimtibu Hazard baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Swansea.
Hali hiyo iliifanya Chelsea kubaki na wachezaji nane uwanjani baada ya mlinda mlango Thibaut Courtois kuzawadiwa kadi nyekundu.Carneiro anaonekana kupoteza nafasi yake kwenye benchi jumapili ijayo katika mchezo dhidi ya Man City baada ya Mourinho kuling'akia benchi lake la huduma ya kwanza kama ''wazembe na wasiojua'' akiongeza kuwa hawakuelewa lolote juu ya mchezo ule.

No comments:

Post a Comment