ROSE
Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na
mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama
mama na mwanaume yeyote.
Akichonga na Amani, Rose alisema japo mume
bora anatoka kwa Mungu na kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini
amechoshwa na hali ya kuishi bila ndoa.
“Mimi kama mwanamke
ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika wakati natamani kuishi
katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na mume wangu na kwa sasa
akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo vigezo ninavyovihitaji,
hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya maisha,” alisema Rose.
Awali
Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ‘King
Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa mwaka jana
waliachana.
No comments:
Post a Comment