BONDIA
Amir Khan amepewa nafasi ya kupigana na Manny Pacquiao Mashariki ya
Kati, wakati Floyd Mayweather akiwa bado hayuko tayari kupigana naye.
Promota
wa Pacquiao, Bob Arum ataanza mazungumzo na uongozi wa bondia huyo wa
Bolton wiki hii kujadili juu ya pambano hilo baada ya kukataliwa na
Mayweather.
Wakati
bondia bora wa mwaka atapigana na Andre Berto mjini Las Vegas Septemba
12, pambano la Khan na Pacquiao, linaweza kufanyika mapema mwakani.
Mtendaji
Mkuu wa The Top amependekeza pambano lifanyike Mashariki ya Kati badala
ya Vegas, ingawa tayari amekataa kulipeleka Dubai.
"Huyu
mtoto Amir Khan anazidi kuchonga kuhusu Manny Pacquiao. Naweza kuandaa
pambano la Khan apigane na Pacquiao,"amesema Arum akizungumza na The Telegraph.
Pac-Man
alilalamika kuumia bega lake kulia wakati anapoteza pambano kwa pointi
mbele ya Mayweather Mei mwaka huu, lakini Arum amesema anaendelea vizuri
na atakuwa tayari kurejea ulingoni mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment