KOCHA
Muingereza Stewart John Hall usiku huu ameiongoza Azam FC kushinda
mechi ya 10 mfululizo tangu arejee kwa mara ya tatu Juni mwaka huu,
baada ya kuifunga KMKM 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao
pekee la Azam FC katika mchezo wa leo limefungwa na beki Gardiel
Michael Kamagi Mbaga kwa shuti la umbali wa mita 14 baada ya pasi ya
Ramadhani Singano ‘Messi’.
Akiichezea
kwa mara ya kwanza Azam FC tangu ahamie kutoka Simba SC mwezi uliopita,
Messi alionyesha kiwango kizuri kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi
ya Yanga SC Agosti 22, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Azam
FC imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya
mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wiki ijayo.
Wapinzani
wao, Yanga SC wameweka kambi Tukuyu, Mbeya na leo pia walikuwa wana
mchezo wa kirafiki, ambao wameshinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons
Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
No comments:
Post a Comment