Tuesday, August 11, 2015

YAYA TOURE AING’ARISHA MAN CITY , YASHINDA 3-0


MABINGWA wa zamani wa England, Manchester City wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu kwa ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo.
Shujaa wa mechi alikuwa na kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure aliyefunga mabao mawili, lingine likifungwa na beki Mbelgiji, Vincent Kompany.
Mwanasoka bora Afrika, Yaya Toure alianza kuifungia Manchester City dakika ya tisa baada ya shuti lake la umbali wa mita 20 kumbambatiza Boaz Myhill na kutinga nyavuni, kabla ya kufunga la pili dakika ya 24.
Nahodha wa Man City, Vincent Kompany akakamilisha ushindi mnono katika mchezo wa kwanza wa timu yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya kwa kichwa 59.  
Mchzeaji mpya, Raheem Sterling aliyesajiliwa kutoka Liverpool, alicheza vizuri katika kikosi cha City jana, lakini akapoteza nafasi nzuri na ya wazi ya kufunga.
Kikosi cha West Brom kilikuwa: Myhill, Chester, Dawson, Lescott, Brunt, Morrison, Gardner, Fletcher, McClean/Yacob dk46, Lambert/Anichebe dk73 na Berahino/McManaman dk79.
Man City; Hart, Sagna, Kompany, Mangala, Kolarov, Toure/Demichelis dk79, Fernandinho, Jesus Navas, Silva, Sterling/Nasri dk73 na Bony/Aguero dk62.

Yaya Toure akifumua shuti kuifungia Man City nbao la kwanza buku kiungo wa Baggies, James Morrison akijaribu bila mafanikio kuzuia

No comments:

Post a Comment