Shirikisho
la Mpira wa Miguu duniani FIFA limepanga kujadili lile sakata la
daktari wa Chelsea Eva Carneiro aliyechimbwa mkwara na kutolewa maneno
machafu pamoja kufungiwa na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.
Caneiro alitolewa maneno makali
na Mourinho baada ya yeye (Caneiro) na Jon Fearn kuingia uwanjani
kumtibia Eden Hazard wakti Chelsea ilipolazimishwa sare ya goli 2-2 na
Swansea ikiwa nyumbani Augost 8 mwaka huu.
Kitendo hicho kilisababisha Eden
kutoka nje ya uwanja na kuwaacha wachezaji wa Chelsea wakibaki tisa
uwanjani kufutia kadi nyekundu aliyooneshwa golikipa wa timu hiyo
Thibaut Courtois.
Kamati ya madaktari ya FIFA
itajadili sakata hilo kwenye mkutano wao Septemba 11 mwaka huu. Kamati
inatarajia kutoa ushirikiano kwa madaktari wa timu wanaofanya kazi
kuhakikisha wachezaji wanakuwa katika hali nzuri.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Michael D’Hooghe amesema: “Huu ni mfano mwingine wa ugumu wa kazi kwa madaktari wa timu”.
“Nataka kujadili suala hili na wenzangu na kuona kama tunaweza kutoa tamko kusaidia madaktari wa timu”.
Mourinho alikosolewa baada ya
mchezo huo kumalizika kutokana na sentensi aliyoitoa kuhusu madaktari wa
timu yake kwenye uwanja wa Stamford Bridge lakini hakurudi nyuma wala
hakuomba radhi.
No comments:
Post a Comment