Wednesday, August 12, 2015

ESPERANCE YAICHAPA 1-0 STADE MALIEN, YAFUFUA NDOTO ZA NUSU FAINALI


TIMU ya Esperance ya Tunisia imefufua matumaini ya kusonga mbele Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia ushindi wa bao 1-0 ugenini jana dhidi ya wenyeji Stade Malien mjini Bamako, Mali.
Shukran kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, Mnigeria, Samuel Eduok huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa ‘Damu na Dhahabu’ na kumaliza wimbi la kufungwa mechi tatu.
Mechi hiyo ya nne ya Kundi A, ililazimika kuchezwa siku mbili baada ya mchezo wa kwanza Jumapili jioni kuvunjika dakika ya 49 kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu eneo la kuchezea Uwanja wa Modibo Keita.
Na kwa mujibu wa sheria, mechi hiyo ikaendelea jana kuanzia pale iliposimamia kwenye Uwanja huo huo na Esperance wakaibuka na ushindi unaompa ahueni Mfaransa Jose Anigo sasa.
Zikiwa zimebaki mechi mbili kukamilisha hatua ya makundi, mabingwa hao mara mbili Afrika wana nafasi ya kwenda Nusu Fainali licha ya kuzidiwa pointi sita na vinara, Etoile du Sahel ya Tunisia pia. Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi saba na Stade Malien ina pointi nne.

MSIMAMO WA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

Kundi A



PWDLGFGAGDPts
1ES Sahel (Tunisia)43013129
2Al Ahly (Misri)42114137
3Stade Malien (Mali)411223-14
4Esperance (Tunisia)410326-43

Kundi B



PWDLGFGAGDPts
1Orlando Pirates43015239
2Zamalek (Misri)43015239
3AC Leopards (Kongo)411224-24
4CS Sfaxien (Tunisia)401315-4

No comments:

Post a Comment