Thursday, August 6, 2015

TFF YASAINI ‘DILI’ LA NGUVU KWA AJILI YA LIGI MSIMU UJAO

Malinzi & MwesigwaShrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu (3) wa udhamini wa ligi kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao na mdhamini mkuu wa ligi hiyo ambayo ni kampuni ya simu za mkonnoni ya Vodacom.
Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amethibitisha kusainiwa kwa mkataba huo lakini akasema hawakufanya sherehe za kutia saini mkataba huo kutokana na  mashindano ya Kagame yaliyokuwa yanaendelea nchini wakati TFF ilikuwa ikiyasimamia kama shirikisho la soka la nchi mwenyeji.
“Kunakitu wanasema katika ajira, unaposikia nafasi haijatangazwa na hajatangazwa mtu mpya jua kwama kuna maendeleo na maranyingi ‘renewal’ ya ‘contract’ huwa hai-sound sana kama tunapoongelea mkataba ambao watu wameingia udhamini mpya”, amesema Mwesigwa.
“Bila shaka mdhami wa msimu wetu unaokuja ni Vodacom ambae tulikuwanae msimu uliopita, kila kitu kimeshawekwa sawa ila kwa maana ya ceremony ndio bado haijafanyika kwasababu kulikuwa na mambo mengi hapa katikati ya Kagame na kadhalika”.
“Mkataba ni miaka mitatu, kutakuwa na maongezeko ukizingatia kuna timu zimeongezeka lakini nadhani hata kile kinachokwenda kwenye vilabu kitaongezeka kwa kiasi fulani yako masuala mengi siwezi kuzungumza kwa undani kwa sasahivi, kwa upande wa kwetu tulikuwa tunayaona hayapo sawasawa. Kulikuwa na muda mwingi sana wakutosha kujadili karibu miezi nane iliyopita kwahiyo kuna vitu vingi vimeangaliwa”.
Kwasababu sherehe ya kusaini mkataba haijafanyika, sitaweza kuingia kiundani zaidi lakini ni mkataba ulioboreshwa ukilinganisha na mikataba iliyotangulia”.

No comments:

Post a Comment