Saturday, August 15, 2015

SIMBA KUIVAA URA YA UGANDA


REKODI YA DYLAN KERR TANGU ATUE SIMBA SC

Simba SC 2-1 Zanzibar Kombaini (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 4-0 Black Sailor (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 2-0 Polisi (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-0 Jang’ombe Boys (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-2 KMKM (Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 1-0 SC Villa (Kirafiki Simba Day)
KOCHA Muingereza, Dylan Kerr leo Jumamosi ataiongoza Simba SC katika mchezo wa saba tangu aanze kazi mwezi uliopita, wakati itakapomenyana na URA ya Uganda.
Mchezo huo wa pili mfululizo dhidi ya timu za Uganda baada ya wiki iliyopita kuifunga SC Villa 1-0, utafanyika pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
Simba ambayo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam, tayari imecheza mechi sita chini ya Kerr na kushinda zote.
Kerr alianza na mechi tano mfululizo Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambazo alishinda 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar, 4-0 dhidi ya Black Sailor, 2-0 dhidi ya Polisi, 3-0 dhidi ya Jang’ombe Boys na 3-2 dhidi ya KMKM.
Wekundu hao wa Msimbazi walirejea Dar es Salaam na kucheza na SC Villa ya Kampala katika kilele cha tamasha la Simba Day, mchezo ambao walishinda 1-0.

No comments:

Post a Comment