Klabu ya Southampton ya Uingereza imakubali kuwa Manchester United
wanavutiwa na wana mpango wa kumsajili winga kutoka nchini Senegal Sadio
Mane. Ieleweke kwamba, United ilifanya jitihada kumapata mchezaji huyo
mwenye miaka 23 tokea juma lililopita lakini Southampton wamekanusha
kupokea ofa yoyote.
Mshambuliaji wa Barcelona Pedro amekuwa
akihisiwa kujiunga na United lakini kwa sasa yupo katika hatua za mwisho
za kijiunga na Chelsea kwa dau la pauni milioni 21.Mane alifunga magoli 10 katika michezo 32 aliyocheza msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu yake ya sasa akitokea Red Bull Salzburg ya Austria na yumo pia katika orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli matatu (hat-trick) kwa muda mfupi zaidi.
No comments:
Post a Comment