Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjani
Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.
Mourinho
aliwakaripia Dakta Eva Carneiro na Jon Fearn kwa kuingia uwanjani huku
timu hiyo ikisalia na wachezaji wachache kufuatia kufurushwa kwa kipa
nambari moja Thibaut Courtois katika mechi ngumu ya kufungua msimu kati
yao na Swansea .Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye alionekana kagongwa kifundo cha mguu.
'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.
''Hii haimaanishi kuwa hawatakuwepo siku nyingine ,katika siku za usoni'' alisema Mourinho.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.
Mourinho aliwataja Carneiro na Fearn kuwa 'wajinga' baada yao kuingia uwanjani kumtibu Hazard katika dakika za lala salama ya mechi ya kufungua msimu.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu.
Mourinho alipoulizwa iwapo anauhusiano mzuri na na kitengo hicho cha utabibu alisema kuwa
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''
'Wenyewe wamenieleza kuwa hawajawahi kushabikiwa zaidi ya kipindi hichi nilipoingia Chelsea''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''
No comments:
Post a Comment