Chelsea ya England imetuma ofa ya euro 60 milion kwa klabu
ya Juventus wakimuhitaji mchezaji wa kiungo, Mfaransa, Paul Pogba, pia
wamepeleka ofa isiyopungua euro 25 milion kwa timu ya Everton ili kumsaini
mlinzi wa kati, Muingereza, John Stones. Ikumbukwe kuwa Alhamis hii timu hiyo
ya London ilikamilisha usajili wa euro 30 milion kumsaini kiungo-mshambulizi wa
pembeni, Mu-Hispania, Pedro Rodriguez kutoka klabu ya FC Barcelona.
“Kwanini, Jose Mourinho amekuwa ‘ kama mwendawazimu’ na kukimbilia sokoni?.’
Jose anaweza kutumia kiasi kisichopungua euro 100 kabla ya
kumalizika wiki hii. Nia yake kuu ni kuwasaini wachezaji watatu wa daraja la
juu ili kushindania mataji ya ligi kuu England na Uefa Champions League ambayo
ni kipaumbele kikubwa kwa mabingwa hao wa EPL msimu wa 2015/16.’
Bila shaka, Mourinho amekitazama kikosi chake katika michezo
miwili ya mwanzo katika ligi ya England kisha kufuatilia ubora wa klabu
nyingine shindani kama, Manchester United, Manchester City, Arsenal na
Liverpool pale England, atakuwa amezichambua pia klabu bora za Ulaya, FC
Barcelona, Juventus, Real Madrid, FC Bayern Munich, PSG, Atletico Madrid na
kugundua wazi kuwa nguvu mpya katika idara za ulinzi, kiungo na ile ya
mashambulizi inaongezeka.
‘Jose anawahitaji wachezaji wote hao na wataipaisha zaidi
endapo watatua Stamford Bridge. Hivyo ndivyo timu bora zinavyosajiliwa, wakati
mwingine klabu zinabidi ziende sokoni kwa gharama kubwa kuwasaini wachezaji
ambao watazuia ‘anguko’ la ndani ya uwanja kwa timu.’
Je, hivi ndivyo klabu za Tanzania zinavyowasaini wachezaji?.
Kamati ya Usajili ya klabu inakuwa na majukumuya moja kwa moja ya kuwasaini ama
kuwatema wachezaji. Haijalishi ni kwa kiasi gani Kamati ya Usajili ya klabu ya
Simba imekuwa ikisaidia kufanikisha usajili wa wachezaji. Majukumu ambayo
kimsingi yanapaswa kufanywa na mwalimu wa timu kutokana na mapungufu ambayo
yamekuwa machoni mwake.
‘ Niambie, nani anayeitaabisha Simba SC kwa miaka ya
karibuni kati ya makocha wanaopata kuifundisha timu hiyo na Watu waliopo katika
Kamati ya Usajili?.’
Nitaendelea kuipinga Kamati ya usajili ya klabu hiyo kwa
kuwa haina uwezo wa kuwasaini ‘wachezaji wa klabu ya Simba’. Kimuonekano,
kiuchezaji, Simba haijawahi kuwa na mchezaji mwili mkubwa. Miili ya wachezaji
kama Mrundi, Kelvin Ndayesenga, Mkenya, Paul Kiongera kiualisia huwa inaendana
na uchezaji wa miaka yote wa klabu.
Simba ni timu ambayo daima inapendelea na imejiwekea ‘ sura
ya uchezaji’ wa kupasiana kutoka idara hadi idara. Kwa maana kiutamaduni
walinzi wanaofanya vizuri katika klabu hiyo ni wale wenye uwezo wa kuusoma
mchezo, kupasiana hata wakiwa katika eneo lao na kupanga mashambulizi yanayotokea
nyuma. Miaka yote ya mafanikio imekuwa ikichezeshwa na wachezaji wenye maarifa
na nguvu za wastani.
Simba si klabu nzuri kwa wachezaji kama Msenegal, Papa Niang
ambaye ametua nchini Ijumaa hii kusaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Muonekano wake tu unaonesha mchezaji ‘atakaye-safa’ katika klabu hiyo licha ya
kukaririwa akisema kuwa ‘ kufunga magoli ndiyo kazi yake’ kuwa mwepesi au uwezo
wa kujipanga katika maeneo ya hatari ili afanikiwe kuthibitisha hilo katika
ligi kuu ya Tanzania Bara. Atakutana na walinzi wepesi ambao mara zote
wanapenda kucheza na majina makubwa ili kuthibitisha ubora wao. Niang huyu wa
Simba atapata wakati mgumu na si ajabu mambo yakawa magumu upande wake.
Upande wangu naamini baada ya ujio wa Musa Hassan Mgosi,
Peter Mwalyanzi na Hamis Kizza kama ‘ wabadala’ wa Emmanuel Okwi, Ramadhani
Singano, Danny Sserunkuma na Elius Maguli, Simba ilimuhitaji zaidi, Ndayesenga,
mchezaji ambaye tayari walitambua uwezo wake. Niang ni ‘ kamari’ tu, si
mchezaji ‘ hulka ya klabu’ kimuonekano,
‘ kiuchezaji sitaraji
mafanikio kutoka kwake na si ajabu akawa mshambulizi chaguo la nne nyuma ya,
Kizza, Mgosi na kijana, Ibrahim Ajib.’
Chaguo la kwanza la kamati ya usajili ya Simba ilikuwa ni
kumsaini, Mrundi, Laudit Mavugo kutoka Vitalo’o ya Burundi lakini timu hiyo ya
‘ Mitaa ya Msimbazi’ katikati ya jiji la Dar es Salaam ilishindwa kufikia dau
lisilopungua milion 100 za Kitanzania hivyo wakakubali kushindwa na kuhamia kwa
Ndayesenga ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Burundi.
Kwa, ‘ Ndaye’ imekuwa mara mbili zaidi kwa maana hiyo Simba
wangelazimika kutumia karibia milion 200 za Kitanzania. Wamenyosha mikono juu
na kumruhusu Mrundi huyo kurejea kwao. Sawa kabisa, naipa 5 timu hiyo kwa
kumtosa, Ndayesenga ila sina hakika na chaguo lao la tatu.
‘ Huyu Niang atakuwa mchezaji wa ‘ bei chee’ ndiyo maana
atasajiliwa na kwa umri anaotembea nao duniani nina shaka na uhalisia wake.
Niang amezaliwa, 07 Octoba, 1988 wakati kaka yake, Mamadou Niang amezaliwa 13
Octoba, 1979.’
0714 08 43 08
No comments:
Post a Comment