SIMBA
SC imefikia makubaliano na wakala Dennis Kadito kuhusu mshambuliaji
Mrundi, Kevin Ndayisenga na sasa mchezaji huyo anakuja kusaini timu ya
Msimbazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba Ndayisenga anarudi kusaini baada ya kumalizana na wakala wake, Kadito.
“Mazungumzo yetu ya awali na Kadito hayakufanikiwa kwa sababu kadha wa kadha. Lakini imekuwa bahati tumerudi mezani tena na tumefikia makubaliano, sasa Ndayisenga anarudi,”amesema Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi lwa Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kuhusu washambuliaji wengie wawili wa majaribio, Makan Dembele wa Mali na Pape Abdoulaye N’daw wa Senegal, Poppe amesema atasajiliwa mmoja wao. “Na si lazima tusajili, tunaweza kuachana na wote iwapo hawataonyesha uwezo wa kuridhisha,”amesema.
N’daw kesho atafanyiwa mtihani wa kwanza wa majaribio wakati Simba SC itakapomenyana na Mafunzo Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakati Dembele anatarajiwa kutua usiku huu.
N’daw anatokea klabu ya Dinamo Bucuresti ya Ligi Kuu ya Romania wakati Dembele anatokea JS Kabyle ya Algeria.

No comments:
Post a Comment