Manchester United wameambiwa wasahau kumsajili Harry Kane, 22, huku
Tottenham wakisisitiza kuwa hawatomuuza mshambuliaji huyo (Guardian),
United huenda wakaweza kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pedro, 29,
ambaye alipachika bao la ushindi katika mechi ya Supercopa, na amedaiwa
kusema anataka kuondoka (Times), meneja wa Arsenal Arsene Wenger
anafikiria kutoa pauni milioni 22 kumtaka kiungo wa Sevilla Grzegorz
Krychowiak, 25 (Daily Telegraph),
Manchester City wamemtaka Kevin De Bryne kutamka wazi kuwa anataka
kuondoka (Manchester Evening News), Chelsea wanajiandaa kumsajili beki
wa kushoto Abdul Rahman Baba, 21, kwa pauni milioni 17 (Sun), Sunderland
watajaribu kumsajili winga wa Manchester United Adnaj Januzaj, 20,
(Sunderland Echo), West Ham wameacha kumfuatilia kiungo wa zamani wa QPR
Joey Burton, 32, baada ya mashabiki kumkataa (MIrror), Torino wanataka
kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 kwa
mkopo na baadaye moja kwa moja (Mirror), Schalke wamesema dau "kubwa
sana" ndio litaweza kuwashawishi kumuuza kiungo wao Julian Drexler, 21
ambaye ananyatiwa na Arsenal na Manchester United (Daily Star), Aston
Villa wanakaribia kumsajili winga kutoka Barcelona Adama Traore, 19, kwa
pauni milioni 12 (Daily Mail), meneja wa Chelsea Jose Mourinho anasita
kumuachia kiungo kutoka Brazil, Ramires, 28 kuondoka huku akinyatiwa na
Juventus (London Evening Standard), QPR watampta mkataba mpya
mshambuliaji wao Charlie Austin iwapo hakuna atakayeweza kumnunua kwa
pauni milioni 15 (London Evening Standard). Share tetesi hizi na wapenda
soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!
No comments:
Post a Comment