Goli la Mussa Hassan Mgosi na
Salumu Gandi limeipa Faru Jeuri ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Stakishari
FC kwenye mchezo Ndondo Cup Sports Xtra chini ya udhamini wa Dr. Mwaka
pamoja na Azam Food Products ikiwa ni hatua ya 16 bora ya michuano hiyo
mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Bandari, Tandika-Temeke, Dar es
Salaam.
Mgosi
alifunga goli hilo kipindi cha kwanza baada ya Faru Jeuri kutawala
sehemu kubwa ya mchezo huo kwa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata
goli la kwanza dakika za mapema za kipindi cha kwanza. Hadi mapumziko
Faru Jeuri walikuwa mbele kwa goli hilo la Mgosi.
Kipindi cha pili kilibadilika
ambapo Stakishari walianza kuliandama lango la Faru Jeuri lakini juhudi
zao zote hazikufanikiwa kuzaa matunda kutokana na ukuta wa Faru Jeuri
kuwa mgumu kupitika.
Wakati Stakishari wakipambana
kusawazisha goli, Faru Jeuri waliandika goli la pili dakika za lala
salama kupitia kwa Salumu Gandi na kuipa Faru Jeuri ushindi wa goli 2-0
mbele ya Stakishari FC na kukata tiketi ya kusonga mbele katika hatua
inayofuta ya michuano hiyo.
Michuano hiyo itaendelea tena
kesho (Jumatano) Agosti 12 kwa mchezo mmoja ambao utawakutanisha Keko
Furniture dhidi ya Buguruni United mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa
Bandari Tandika-Temeke.
No comments:
Post a Comment