Mlinda
mlango wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Thibaut Courtois
ataukosa mtanange dhidi ya Manchester City baada ya rufaa yake dhidi ya
kadi nyekundu alioipata katika sare ya 2-2 dhidi ya Swansea kukataliwa.
Mlinda
mlango huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye miaka 23, alitolewa nje
alipomzuia mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis nafasi ya kufumania
nyavu katika mchezo uliopigwa jumapili darajani Stamford.Chama cha soka cha uingereza FA, kimesema Chelsea imeshindwa kuthibitisha kuwa mwamuzi Michael Oliver alifanya makosa katika mchezo huo.pamoja na hayo Asmir Begovic aliyesajiliwa katika majira ya kiangazi kutoka Stoke City anatarajiwa kusimama langoni dhidi ya City.
Chelsea mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza wanatarajiwa kuwakabili Man City walioshika nafasi ya pili msimu uliopita jumapili hii katika uwanja wa Ethihad.
No comments:
Post a Comment