Sunday, August 30, 2015

Ssentongo awaita mezani Simba


UNAKUMBUKA Robert Ssentongo? Huyu jamaa kwasasa ndiye mtambo wa mabao katika kikosi cha URA ya Uganda.

Miaka kumi iliyopita alikuwa akisakata soka pale Msimbazi, katika kiwango cha juu kabisa, lakini pilikapilika za pale zikamtoa nje akaondoka.

Miaka kumi baadaye mchezaji huyo yuko katika kiwango kile kile, akiwa na makali yaleyale.
Ssentongo amesikia Simba wanasaka straika wa maana wa kuwatoa kamasi mabeki na kufunga mabao, akacheka kidogo, kisha akauliza; “Mimi hawanioni?”.

Ssentongo amesema kwamba anakaribisha ofa kutoka Simba kwasababu ni timu anayoipenda, na kwamba kama watakubaliana anaweza kusaini Simba na akaifanyia makubwa.

“Najua muda wenyewe umemalizika, lakini kama wangekuja mapema tukaongea ningejiunga na Simba, nikaanza maisha mapya. Mimi najitambua kwamba ni aina ya washambuliaji ambao Simba inawataka kwasasa”, amesema.

Mshambuliaji huyo ambaye mwaka 2009 alirejea tena Tanzania na kujiunga na African Lyon amesema kwamba pamoja na kwamba amesakata soka kwa muda mrefu, lakini kiwango chake kiko juu.

Murshid ampagawisha Micho


KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Uganda “The Cranes”, Milutin 'Micho' Sredojević amesema kiwango cha beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid ni kikubwa mno.

Kocha huyo raia wa Serbia aliyewahi kuinoa Yanga ya Tanzania, amesema kwamba kiwango cha beki huyo wa Simba kimekuwa kikiongezeka kila siku, na akakiri kwamba anaweza kuwa beki bora katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Namjua Juuko, naona kila siku kasi yake inaongezeka. Anaonekana kuna mambo ameongeza sana katika soka lake ndio maana nimelazimika kumwita katika timu ya taifa” amesema Micho.

Ameisifu Simba kwa kumwongezea makali beki huyo akisema kwamba kila anaporejea Uganda anakuwa na vitu vipya kabisa.

“Ingawaje watu wengi wanasema kwamba ndiye beki katili na mtukutu zaidi katika Uganda na Afrika Mashariki pia, lakini kwangu mimi naona kwamba hiyo ndiyo staili yake ya kuzuia washambuliaji wakali”, amesema kisha akaongeza;

“Hata hivyo huwa namwambia kwamba anapocheza mpira lazima ahakikishe kwamba rafu zake hazileti madhara kwa timu. Nadhani hata huko Simba, rafu zake hazijaigharimu kabisa timu, vinginevyo asingekuwa chaguo la kwanza la mwalimu” amesema.

Kocha huyo amesema kwamba siku zote mwalimu makini humtazama na kumpenda beki ambaye anaogopewa na washambuliaji wakorofi pia.

“Kwangu mimi nampenda Murshid kwa staili yake ya kuwadhibiti washambuliaji wanaoitwa wakorofi. Hii ndiyo beki ya kazi” alitamba.

Kimwaga: Nitaonesha makali Simba


KIUNGO mpya wa Simba, Joseph Kimwaga amekiri wazi kuwa alikata tamaa ya kucheza mpira baada ya mambo kuwa magumu katika klabu ya Azam FC, lakini sasa ataonesha makali yake.

Kimwaga licha ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Azam FC alisumbuliwa na majeraha ya goti kiasi cha kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

Mchezaji huyo anayetumia mguu wa kushoto anakumbukwa na wapenzi wengi wa mpira nchini kutokana na kufunga goli la ushindi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Novemba, 2013 wakati Azam iliposhinda 3-2.

“Baada ya kuumia na kuwa nje kwa muda mrefu nilianza kukata tamaa kama kweli ningeweza kurudi katika kiwango changu cha kawaida. Kusajiliwa na Simba nitachukulia kama njia ya kurejesha makali yangu” anasema Kimwaga kwa njia ya simu akiwa kambini Zanzibar.

Simba imekuwa Zanzibar kwa kambi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi kuu Septemba 12, itacheza na JKU ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili hii.

Kimwaga tayari amecheza gemu moja ya maandalizi wakati timu hiyo ilipotoka sare ya bila kufungana na Mwadui FC wiki iliyopita anatajwa kama mtu wa kuchukua nafasi iliyoachwa na winga Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye amejiunga na Azam FC.

“Nipo hapa kufanya kazi, lengo langu ni kushirikiana na wenzangu kuisaidia Simba msimu huu. Najifua ili kumshawishi mwalimu nipate nafasi ya kucheza mara kwa mara. Unajua nimekuwa nje ya uwanja kwa mwaka mzima kutokana na majeraha. Anasema Kimwaga ambaye tangu amepona hakuwahi kuichezea Azam FC katika mechi ya ushindani.

Simba wapewa dozi mara mbili Zanzibar



WEKUNDU wa Msimbazi, timu ya soka ya Simba wako katika mazoezi ya mwisho kabla ya kuingia katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Simba wameweka kambi katika mji ambao wana bahati nao wa Zanzibar, na mazoezi yanayoendelea hapa tangu wametua juzi, ni sawa mgonjwa anayepewa dozi kutwa mara mbili.

Na kama kawaida yao, Wekundu hao wamekuwa wakifanya mazoezi hayo katika uwanja wa Amaan, muda wa asubuhi na jioni.

Kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola amesema mazoezi yanakwenda vizuri, na wataitumia michezo ya wikiendi hii ya kirafiki kama kipimo cha kuwanoa na kuwatazama wachezaji wake kwa mara nyingine.

“Tumeanza mazoezi vizuri tunatarajia kukaa hapa mpaka tarehe 9 ya mwezi ujao, pengine siku hiyo tutarejea bara tayari kucheza ligi kuu”, alisema Matola.

Kuhusu wachezaji wawili wa kigeni ambao simba wanatarajia kumchagua mmoja atakae wafaaa Matola amesema mmoja ameshafika visiwani na mmoja alitarajiwa kufika wakati wowote. Wachezaji ambao ni Pape na Ndembele, mmoja raia wa Mali na mwengine ni Msenegal.

“Ndio maana tunacheza michezo miwili ya kirafiki, dhidi ya JKU na Mafunzo ambao ndio mabingwa wa ligi kuu soka Zanzibar ili tuweze kuchagua mmoja anayetufaa”, amesema Matola.

Hata hivyo Simba inawakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu walioko katika timu ya taifa ya Tanzania pamoja na ile ya Uganda.

Beki wake katili, Juuko Murshid hayuko katika kikosi kilichoko Zanzibar kwasababu ameitwa kwenye timu ya taifa ya Uganda, “The Cranes”. Walioko katika timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” ambayo imepiga kambi nchini Uturuki ni mabeki Hassan Isihaka, Mohammed Hussein “Tshabalala”, viungo Abdi Hassan Banda na Saidi Ndemla pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

Kiongera mambo saafi Msimbazi


PAUL Kongera
KAMA kuna anayedhani Wekundu wa Msimbazi hawana mpango na Paul Kiongera, hiyo itakuwa imekula kwake! Kwa taarifa yako tu, Straika huyo raia wa Kenya bado ni mali halali ya klabu ya Simba.

Lakini siyo hilo tu, kinachotakiwa kujulikana hapa ni kwamba, klabu ya Simba imepanga kumjumuisha kikosini ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Haya yamebainishwa na Rais wa klabu ya Wekundu hao,Evans Aveva alipolitolea ufafanuzi suala la mpachika mabao huyo ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika tmu ya KBC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya.

Akiweka bayana, Aveva alisema, Kiongera bado ana mkataba na Simba na ndiyo maana ililazimika kumtoa kwa mkopo kwa timu hiyo ya Kenya.

Aveva alilazimika kutoa ufafanuzi suala la straika huyo baada ya kuwapo kwa ushauri wa wanasimba wanaoutaka uongozi kumrejesha kikosini mchezaj huyo katika kipindi hiki ambacho kocha Dylan Kerr anahaha kupata mfumania nyavu wa maana.

Akijibu, Aveva alisema, straika huyo ni mali yao na kwamba mwezi Desemba atarejea Msimbazi kama mchezaji halali na kuendelea na kandarasi ya kuitumikia klabu.

"Kiongera bado ni mchezaji wetu halali, tulimtoa kwa mkopo KBC kwa makubaliano maalum, hivyo lazima tuyaheshimu na kandarasi yake ya kucheza kwa mkopo itakoma mwezi Desemba mwaka huu" amenukuliwa rais huyo wa Simba.

Kiongera alisajiliwa na Simba msimu uliopita, lakini bahati mbaya hakudumu baada ya kuandamwa na majeraha mwanzoni kabisa mwa msimu alipoumia katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Coastal Union, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

'Simba ni ya mvua na jua'


KOCHA Dylan Kerr amewaambia wachezaji wake jambo moja kubwa, ambalo ni hili:" Timu hii ni ya mvua na jua.Anayezembea mazoezi kwasasa imekula kwake na hana haja ya kubakia na wachezaji wavivu".

Lakini, kama vile haikutosha, Kerr alionesha kutotaka mzaha katika kusimamia mazoezi hayo kwa vitendo huku mwenyewe akiwa mfano wa kila hatua ya kujifua kwao.

Katika hali ya kutaka kukiweka sawa kikosi chake kabla ya kuanza kwa ligi ya msimu unaotarajia kuanza Septemba 12, Kerr alikiongoza kikosi chake bila kujali hali ya hewa iliyokuwapo kisiwani hapa juzi Ijumaa.

Mazoezi ya juzi Ijumaa yaliyofanyika katika uwanja wa Amaan, kocha Kerr aliwaongoza wachezaji wake kwa kuendelea kujifua huku kukiwa na hali ya hewa tete ya mvua kubwa iliyonyesha kuanzia asubuhi.

Wakati ambapo baadhi ya waliohuhudhuria mazoezi hayo wakidhani 'mziki' wa mazoezi utasimama kutokana na mvua hiyo,Kocha Dylan Kerr aliwaambia wachezaji wake 'Zege halitolala'.

Lakini, katika mazingira ya ajabu, wachezaji nao wakaonesha kuwa 'ngangari', wakafurahia hali hiyo na kuendelea na tizi la nguvu hali ambayo iliwapa raha makocha wote watatu.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo,Kerr alisema, amefurahia hali ya hewa iliyopo Zanzibar kwasasa, kwani inawapa changamoto wachezaji ya kujifua katika mazingira ya aina mbalimbali.

Alisema, wachezaji ni sawa na maaskari wa jeshi la ukombozi wanaopaswa kuwa tayari kufanya kazi katika mazingira yoyote kwa ajili ya kulinda heshima na ushindi wa nchi yao.

Aliongeza kuwa, amelazimika kuendelea na mazoezi katika mazingira ya mvua kwasababu timu lazima ijiandae kwa mazingira yoyote magumu na rahisi, kinachotakiwa ni kuwajengea utayari na stamina.

"Timu ni kama kikosi cha askari. Lazima wawe tayari kwa mazingira yoyote kwa ajili ya kupigania hadhi, heshima na ushndi kwa ajili ya wenzao ambao ni wanachama na washabiki wa klabu ya Simba" alisisitiza Kerr.

Kikosi hicho Dylan Kerr kipo kisiwani Ungujakujiandaa na Ligi Kuu ya msimu huu inayotarajia kuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu ambapo itafungua pazia dhidi ya African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Ndayisenga akubali kutua Simba


SIMBA SC imefikia makubaliano na wakala Dennis Kadito kuhusu mshambuliaji Mrundi, Kevin Ndayisenga na sasa mchezaji huyo anakuja kusaini timu ya Msimbazi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba Ndayisenga anarudi kusaini baada ya kumalizana na wakala wake, Kadito.

“Mazungumzo yetu ya awali na Kadito hayakufanikiwa kwa sababu kadha wa kadha. Lakini imekuwa bahati tumerudi mezani tena na tumefikia makubaliano, sasa Ndayisenga anarudi,”amesema Poppe.

Kuhusu washambuliaji wengie wawili wa majaribio, Makan Dembele wa Mali na Pape Abdoulaye N’daw wa Senegal, Poppe amesema atasajiliwa mmoja wao. “Na si lazima tusajili, tunaweza kuachana na wote iwapo hawataonyesha uwezo wa kuridhisha,”amesema.

N’daw jana alifanywa mtihani wa kwanza wa majaribio wakati Simba SC ilipomenyana na JKU Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakati Dembele alitarajiwa kutua jana .

N’daw anatokea klabu ya Dinamo Bucuresti ya Ligi Kuu ya Romania wakati Dembele anatokea JS Kabyle ya Algeria.

Simba yafunga usajili na wawili

DIRISHA la Usajili kwa timu za Ligi Kuu Tanzania bara linatarajia kufungwa Jumapili (Leo) saa 6:00 usiku huku uongozi wa klabu ya Simba ikitangaza kukamilisha kumalizana na wachezaji wawil raia wa kigeni.

Taarifa za uhakika ambazo Mwanasoka linazo zimebainisha kuwako kwa hatua za mwisho za uongozi wa Rais wa klabu hiyo, Avans Aveva kukamilisha mazungumzo ya kuwasainisha wachezaji hao wawili wa maana.

Akinukuliwa jana, bila ya kutaja majina ya wachezaji hao, Aveva alizungumza kwa uhakika mkubwa kuwa, wachezaj hao ni wale watakaokubalika pia na benchi la ufundi ambalo ndilo lililo na jukumu la kuamua nani asajiliwe na yupi wa kuachwa.

Rais huyo, alisema, uongozi una masaa machache ya kupokea baraka za benchi la ufundi juu ya wachezaji hao kabla ya kuweka bayana majina ya wachezaji hao na kuungana na wenzao ambao tayari wameshasaini kandarasi ya kukukipiga Msimbazi msimu mpya wa ligi.

Ingawa ni mapema mno, lakini mwandishi wa habar hizi amebainishiwa majina yao na kuumbwa kubakia kuwa ni suala la siri hadi hapo kila kitu kitakapokwenda sawia bin sawa.

Pamoja na usiri huo, Mwanasoka linatambua kuwapo kwa majina ya wachezaji wawili raia wa kigeni ambao tayari wapo katika malengo ya kusajiliwa baada ya kufuzu majaribio chini ya kocha Dylan Kerr.

Wachezaji waliomo ndani ya kurunzi za majaribio katika kambi ya Wekundu hao kisiwani Unguja ni pamoja na Pape Abdoulaye N'Daw ambaye tayari ameanza kuangalia kiwango, huku mwenzake Makan Dembele alitarajiwa kutua viswani humo muda wowote.

"Tutakamilisha usajili wetu katika ubora mkubwa ila kwa kupata baraka za kocha wetu Dylan Kerr ambaye ndiye anayesubiriwa, lakini kila kitu kinakwenda sawa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji wa kigeni".

"Tunaamini kila mwanasimba atafurahia kikosi cha msimu huu na hilo ndilo linaufanya uongozi kuwa kufanya mambo yake katika umakin mkubwa kwa kusikiliza maoni ya makocha wetu Kerr (Dylan) na Matola (Seleman)".

Alinukuliwa mjumbe mmoja wa kamati ya usajili ambaye hata hivyo hakutaka jina lake liandikwe kwasababu ya kuheshimu mipaka ya majukumu.

Akizungumzia masuala ya ufundi, mjumbe huyo alisema, wachezaji wote wawili wana uwezo wa kufunga mabao ya masafa marefu, sifa ambayo imewavutia makocha wote wawili

Saturday, August 29, 2015

Twiga Stars kuanza na Ivory Coast michezo ya Afrika

 TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Kongo- Brazzaville kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
Twiga Stars iliyoweka kambi kisiwani Zanzibar kwa takribani mwezi mmoja sasa, itacheza mchezo wake pili Septemba 9, dhidi ya Nigeria kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Congo-Brazzavile Septemba 12, 2105.
Jumla ya timu nane za Wanawake kutoka Barania Afrika zinashirki fainali hizo ambazo ni Nchi za Afrika Kusini, Cameroon, Ghana, Misri (wamejitoa) kundi B, na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast, Nigeria na Tanzania kutoka kundi A.
Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Stars yalala kwa Libya, Bocco ang'ara

Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 2-1 leo na Libya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya The Green Park mjini Kartepe, Uturuki. Bao la Stars inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa lilifungwa mshambuliaji John Bocco 'Adebayor'. 
Stars imeweka kambi Uturuki kujiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria Septemba 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam.

Ndayisenga anarudi kusaini Simba, wakala wake athibitisha



SIMBA SC imefikia makubaliano na wakala Dennis Kadito kuhusu mshambuliaji Mrundi, Kevin Ndayisenga na sasa mchezaji huyo anakuja kusaini timu ya Msimbazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba Ndayisenga anarudi kusaini baada ya kumalizana na wakala wake, Kadito.
“Mazungumzo yetu ya awali na Kadito hayakufanikiwa kwa sababu kadha wa kadha. Lakini imekuwa bahati tumerudi mezani tena na tumefikia makubaliano, sasa Ndayisenga anarudi,”amesema Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi lwa Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kuhusu washambuliaji wengie wawili wa majaribio, Makan Dembele wa Mali na Pape Abdoulaye N’daw wa Senegal, Poppe amesema atasajiliwa mmoja wao. “Na si lazima tusajili, tunaweza kuachana na wote iwapo hawataonyesha uwezo wa kuridhisha,”amesema.
N’daw kesho atafanyiwa mtihani wa kwanza wa majaribio wakati Simba SC itakapomenyana na Mafunzo Uwanja wa Amaan, Zanzibar, wakati Dembele anatarajiwa kutua usiku huu.
N’daw anatokea klabu ya Dinamo Bucuresti ya Ligi Kuu ya Romania wakati Dembele anatokea JS Kabyle ya Algeria.

Henry atoa maneno mazito

Thierry Henry Barcelona

Thiery Henry: “I went to sleep knowing what to do. I always thought if I don’t move, Abidal won’t, Iniesta won’t get the ball. It’s constant.”
Hayo Ni maneno ya Thierry Henry Na Mimi Yamenikosha sana  na nimeona ngoja nitie maneno yangu  kuzungumzia kuhusu mpira wa miguu…
Unajua kwa sisi mashabiki wa mpira tunaishia tu kujua kuhusu formation za team labda sana ukijitahidi utajua kuhusu filosofi flani ya timu flani basi hapa tumekua tumeridhika na tuna-enjoy mpira kwa kiasi kile  tunachouelewa …
Ila mpira kama mpira una utaalamu wake ambao watu wengi  hua hatuufahamu wala hatujishughulishi kuujua ambao labda utaalamu huu ungeweza kutubadili mawazo na kutuongezea sana radha ya soka.
Kitu kinacholeta ladha ya mpira na utofauti wa timu moja na nyingine sio tu pekee filosofi ya timu na wala sio tu formation pekee inayotumiwa na timu .. utofauti wa team moja hadi nyingine unaletwa na jinsi gani utautembeza mpira wenu kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutumia watu gani na ni kwanini mtu au watu hao  ndio watumike, kumbe basi timu zinaweza kushare formation moja, na pia zinaweza kushare filosofi moja ya mpira ila bado njia zao za kupitisha hiyo mipira kutoka eneo moja hadi lingine zikawa tofauti.
Na kutokana na hili suala ndio maana kuna muda hata zile team kubwa zenye wachezaji wazuri hua zinafungwa. Kinachowafanya wafungwe hapa sio formation na wala sio kwakua mchezaji flani anacheza mahali flani ndio maana timu imefungwa kwakua sio nafasi yake, bali kinachofanya kupoteza mechi ni mbinu za kupitisha mipira za timu husika ilioshinda.
Ukisikia neno ‘Game Plan’ hua haliishii tu kwenye formation na filosofi za timu basi, kama ingekua inaishia hapa basi makocha wenye experience zao au wale high profile managers wasingekua wanajisumbua kwenda uwanjani kuisoma timu pinzani ikicheza na timu nyingine kwakua kutokana na experince zao wangeelewa tu wacheze nazo vipi hizo timu wakikutana nazo kwakua mara nyingi hua wanajua vitu vingi sana kweye soka.
Na pia mnaweza mkakutana na timu mbili tofauti mnacheza mpira unaofanana na formation inayofanana ila bado matokeo yakawa tofauti hii ni kutokana na hamuwezi kufanana njia za kupitisha mipira wachezaji mnaotumia kuanzisha mashambulizi wapo kwenye position zipi na pia ni mchezaji gani anaanza kukaba wapi, hadi kufika wapi mnaanza kungia kwa nguvu kuchukua mpira, mnaiba vipi muda kuvizia kuanzisha shambulizi hamuwezi kufanana hivi vitu.
Makocha wanakua wana njia nyingi za kuwaambia wachezaji wao wapitishe mipira kutokana mechi husika pamoja na uwezo wa wachezaji waliokuwepo uwanjani siku hiyo, hivyo basi kila mechi hasa hizi mechi muhimu hua zina game plan yake ya tofauti ambayo hii ni zaidi ya kuona formation uwanjani. Makocha wanaamua kwenda viwanjani kuangalia mpinzani anavyocheza  kwakua huwez kuiona game plan ya mpinzani wako kwenye TV kwakua TV zinaonesha tu sehemu ambao mpira ulipo.
Mpira hua unachezwa sehemu mbili yule anaekua na mpira kwa wakati huo pamoja na wale wasiokua na mpira ina maana positioning zao ni jinsi gani timu inajipanga kama mpira wanao wao,  ni mchezaji gani hua anakimbia kwenye eneo gani kama team yake ina mpira hivi ndio vitu ambavyo makocha au scouts wanaenda kuvitazama uwanjani ambavyo huwezi kuviona kwenye TV, TV itakuonesha mpira ulipo mara mchezaji kapokea pasi alipotokea huwezi kuona labda hadi replay .
Henry anakwambia alikua anaenda kulala akijua kua ili Abidal aweze kuachia mpira miguuni mwake lazima yeye awe amefika eneo fulani na asipofika hilo eneo ina maana Abidal hawez kuachia mpira hapa ikumbukwe kua mpira huu ambao upo kwa Abidal hautoki miguuni kwa Abidal moja kwa moja hadi kwa Thierry Henry la hasha ila unapitia kwa Iniesta ambae nae kwa wakati huo anakua hana mpira kwakua mpira upo miguuni kwa Abidal.
Mpaka hapa kuna kua kuna watu watatu wanacheza mpira mmoja ambao upo miguuni mwa mtu mmoja tu ambae ni Abidal.
Kama Thiery Henry asipofanya hii move anaweza kuisababishia timu yake iwe in trouble kwakua anaweza kufanya Abidal asifanye maamuzi sahihi kama ilivyokua planned, kwaiyo Henry akifanya move yake na Iniesta yeye kazi yake inakua kumtupia tu Henry kwakua anajua ni wapi alipo, hapa sasa Iniesta anaweza akakupumbaza labda kwa kupiga chenga mbili tatu ili akushawishi kua ana mpa Henry labda tu kwakutaka kuuachia mpira miguuni mwake kwakua amekabwa kumbe anakua anakudanganya Thierry Henry ndio anakua mtu sahihi alitaka kumpa.
Hapa ndio mpira hua unachezwa na ndio maana kwa watu wenye uelewa haachi kwenda kuangalia mpira uwanjani hata kama unaoneshwa kwenye TV kwakua akienda uwanjani anaona mchezo mzima ulivyo.
Hizi formation zipo ili tu wachezaji wakae kwenye system flan ila kinachofanya team ifungwe au ipate ushindi sio tu formation pekee mpira hua hauishii hapo ni ile game plan ndio inayosababisha timu kufungwa au kushinda.
Kuna muda unaweza kuona timu ile ile moja na wachezaji wanajipanga vile vile kwenye mechi kama tano mfululizo na mechi zote timu hiyo hiyo moja kwa kikosi kile kile inapata matokeo ya ushindi, kumbe basi hapa wanachokua wanabadilisha ni jinsi gani ya kucheza, kupitisha ile mipira yao wakati wa kushambulia na style yao ya kuzuia wakati wa kukaba.
Kwa maana hii basi ni kwamba hamna timu yeyote duniani hata kama iwe bora kiasi gani inayoweza kucheza yenyewe tu bila mwalimu wa kuwaelekeza, na ndio maana hata wale wachezaji magwiji kabisa waliowahi kuwa bora duniani hua na wao wanaenda kusomea kua walimu wa mpira.
Sisi mashabiki wa mpira tunakua rahisi mno kusema na kulalamika “mchezaji flani hawez kucheza kama mchezaji wetu flani, mara me huyu flani anaudhi sana kocha nae kwanini hamtoi anaendelea tu kumpanga mi naudhika” *** tambua kama hata wewe umeona flani hawezi kucheza kama flani aliekua benchi basi ujue hata mwalimu anaewafundisha wachezaji hao amewaona na anawajua kuwa flani hajui kufanya kitu hiki na isitoshe anakua nao kila siku mazoezini.
Makocha wote duniani wanaangalia zaidi game plan zao kuliko uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, ndio maana kwa wanaojua soka wanakwambia kujua mpira na kudumu kwenye mchezo wa mpira sio kipaji tu unaweza ukawa na kipaji na usifike popote, muhimu ni kufanya mazoezi kujituma sana na kuwa na nidhamu kweli kweli nje na ndani ya uwanja na pia kufata maelekezo ya mwalimu hapa utafanikiwa kimpira.
Ukimkuta mchezaji mwenye kipaji cha ukweli, na ana nidhamu ya hali ya juu anafanya mazoezi kisawasawa na kusikiliza walimu wao hawa ndio hua wanafanikiwa mno.
Kwaiyo ushauri wangu kwa watu wa mpira ni kwamba, tunapoenda kuangalia mpira kabla hujaanza kulalamika kwanini flani anachezeshwa hivi kwanini flani hachezi na kuanza kukasirika, jaribu kutafakari kwanza ni nini kocha ana hitaji kutoka sehemu hiyo, kama ukitafakari na ukaelewa labda inaweza kukusaidia kuenjoy huo mchezo badala ya kukasirika na itakusaidia pia kuelewa.
Na hata hao wanaokua nje haina maana watakaa nje forever, kuna wakati inakua wanakua wanamechi zao watacheza au labda pia walimu wao wanakua wanawatafutia njia ya kuwaingiza kikosi cha kwanza bila kuharibu muendelezo wa timu.
Naishia hapa namalizia kwakusema kua nimekoshwa sana na maneno ya Thiery Henry sentensi chache tu ila zimebeba maana nzima ya football.

Fifa sasa yaingilia kati sakata la Mourinho na daktari wa Chelsea

carneiro vs mourinhoShirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA limepanga kujadili lile sakata la daktari wa Chelsea Eva Carneiro aliyechimbwa mkwara na kutolewa maneno machafu pamoja kufungiwa na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.
Caneiro alitolewa maneno makali na Mourinho baada ya yeye (Caneiro) na Jon Fearn kuingia uwanjani kumtibia Eden Hazard wakti Chelsea ilipolazimishwa sare ya goli 2-2 na Swansea ikiwa nyumbani Augost 8 mwaka huu.
Kitendo hicho kilisababisha Eden kutoka nje ya uwanja na kuwaacha wachezaji wa Chelsea wakibaki tisa uwanjani kufutia kadi nyekundu aliyooneshwa golikipa wa timu hiyo Thibaut Courtois.
Kamati ya madaktari ya FIFA itajadili sakata hilo kwenye mkutano wao Septemba 11 mwaka huu. Kamati inatarajia kutoa ushirikiano kwa madaktari wa timu wanaofanya kazi kuhakikisha wachezaji wanakuwa katika hali nzuri.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Michael D’Hooghe amesema: “Huu ni mfano mwingine wa ugumu wa kazi kwa madaktari wa timu”.
“Nataka kujadili suala hili na wenzangu na kuona kama tunaweza kutoa tamko kusaidia madaktari wa timu”.
Mourinho alikosolewa baada ya mchezo huo kumalizika kutokana na sentensi aliyoitoa kuhusu madaktari wa timu yake kwenye uwanja wa Stamford Bridge lakini hakurudi nyuma wala hakuomba radhi.

Friday, August 28, 2015

Messi Mwanasoka bora Ulaya


NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amempiku hasimu wake mkubwa, Cristiano Ronaldo na mchezaji mwenzake wa Barca, Luis Suarez katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya msimu wa 2014-15.
Messi ameshinda tuzo hiyo mwa mara ya pili katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Monte Carlo mjini Monaco, Ufaransa jana jioni baada ya kupangwa kwa ratiba ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujeruman, Celia Sasic ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Mwaka Ulaya akiwa tayari ametangaza atastaafu soka tangu mwezi uliopita. Sasic amewapiku mchezaji mwenzake wa Ujerumani, Dzsenifer Marozsan na Amandine Henry wa Ufaransa alioingia nao fainali.
Lionel Messi akifurahia na tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa mjini Monaco, Ufaransa.

Usain Bolt bingwa wa dunia wa mita 200


Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.
Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.
Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na
Gatlin alitumia sekunde 19.74.
Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa Bahamas akiridhika na medali ya fedha.
Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99.
Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada, Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mchujo.
Hata hivyo Sum, alinusurika pale muda wake wa dakika 1.57.56 ulikuwa wa kasi zaidi kati ya wale waliomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao, na hivyo kufuzu kwa fainali.

Demu wa Balotelli sasa apata njemba mpya

BENEZA
Mario Balotelli alikua kwenye mapenzi na huyu model kiasi kwamba walifikia hadi level ya kuvishana pete wakikaribia kufunga ndoa. Lakini mapenzi yao yakaishia kusambaratika na kila mtu kuchukua hamsini zake.
Mrembo huyo ambae ni model kutoka Belgium hajaenda mbali sana na aina ya mpenzi wake wa zamani. Hivi model Fanny Neguesha anatoka na mchezaji wa West Ham Cheikhou Kouyate na mapenzi yao yanaoenekana kuwa mazito sana hivi sasa.
Model huyu mwenye miaka 25 hajachelewa kuweka wazi mapenzi makubwa kwa baby wake ambapo amekua aki-post picha nyingi sana kwenye instagram ndani ya jezi yaWest Ham. Pia ali-post dessert ambayo imeandikwa jina la msenegal huyo Cheikhou Kouyate na kuandika caption ya Best Friend for Life.
we
2BB30AE900000578-3212593-Belgian_model_Fanny_Neguesha_has_worn_a_West_Ham_United_away_shi-m-8_1440667538927
2BB3184F00000578-3212593-image-a-6_1440667419298
2BB30AF900000578-3212593-image-a-9_1440667658976

Makundi ya Ligi ya mabingwa Ulaya 2015/16

COVEER
Haya ndo makundi ya Ligi ya mabingwa Ulaya

A :
  • PSG
  • REAL MADRID
  • SHAKHTAR DONETSK
  • MALMO
B:
  • PSV
  • MAN UNITED
  • CSKA MOSOW
  • WOLFSBURG
C :
  • BENFICA
  • ATHELICO MADRID
  • SHAKHTAR DONETSK
  • ASANTA
D :
  • JUVENTUS
  • MANCHESTER CITY
  • SEVILLA
  • BORUSSIA MONCHENGLADBACH

E :
  • BARCELONA,
  • BAYERN LEVERKUSEN
  • ROMA
  • BATE BORISOV
F :
  • BAYERN MUNICH
  • ARSENAL
  • OLYMPIACOS
  • DINAMO ZAGREB
G :
  • CHELSEA
  • PORTO
  • DYNAMO KIEV
  • MACCABI TEL-AVIV
H :
  • ZENIT ST PETERSBURG,
  • VALENCIA,
  • LYON
  • GENT

Pistorius kuendelea kukaa gerezani zaidi

Kamati itakayoamua ikiwa mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anapaswa kuachiliwa kutoka gerezani, inatarajiwa kukutana tarehe 18 mwezi ujao.
Waziri wa haku nchini humo, alizuia mwanariadha huyo kuachiliwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Waziri huyo amesema kuwa uamuzi wa kamati hiyo ya kutoa msamaha wa kumuachilia mwanariadha huyo, baada ya kutumikia kifungo cha miezi kumi ya kifungo chake cha miaka mitano ulitolewa mapema na haina msingi wowote.
Mahakama nchini humo ilimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka wa 2013.
Pistorius alimpigia risasi Steenkamp akiwa bafuni nyumbani kwake mjini Pretoria, baada ya kumshuku kuwa ni mwizi.
Upande wa mashitaka umekataa rufaa ya hukumu hiyo ukisema kuwa Pistorius anapaswa kuhukumiwa kwa mauaji.
Mawakili wa Pistorius wanatarajiwa kuwasilisha nyaraka zao kupinga rufaa hiyo tarehe 17, mwezi ujao, siku moja tu kabla ya kamati hiyo ya kutoa msamaha kukutana.

Everton yakataa ombi la John Stones kutua Chelsea


stonesssss
Licha ya klabu ya Everton kupelekewa ofa tatu na Chelsea za pauni milioni 20, 26m na 30 kwa ajili ya beki wao John Stones,pia beki huyo kupeleka barua ya kuomba kuondoa klabuni hapo, bado club ya everton imeendelea kukataa kumuuza mchezaji huyo.
Kupitia tovuti ya klabu hiyo mwenyekiti wa club hiyo Bill Kenwright amesema “club ya Everton imekataa ombi la John stones la kuhamia klabu nyingine, tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili tumekataa ofa mbalimbali kwa ajili ya John”.
Akamalizia kwa kusema “John sio wa kuuzwa na atabaki kua mchezaji wa muhimu katika timu yetu”.
Kocha wa Everton alipoulizwa kuhusu kukataliwa kwa ombi la John alisema “Bado hatujalikataa sababu leo ni siku ya mechi na suala la kuhama halikua kipaumbele chetu.Tutalikataa asubui na kuendelea na shughuli zetu.”

Thursday, August 27, 2015

Niang aondoka kwa huzuni Simba


PAPA Niang
STRAIKA raia wa Senegal ambaye alitua Simba na kujaribu kufanya majaribio, kisha akatupiwa virago baada ya siku moja Papa Niang, ameondoka na kusema wazi kwamba mpira wa Tanzania ni mgumu.

Nianga ambaye Simba imemrejesha kwao baada ya kushindwa kuonesha makeke aliyotarajiwa kuyafanya katika mechi ya kirafiki kati ya Simba na Mwadui FC ya Shinyanga iliyomalizika kwa sare tasa, amesema kwamba ameshindwa kutamba kutokana na mfumo mgumu wa soka aliloshuhudia.

Amesema kwamba mfumo wa soka la Tanzania ni mgumu sana kwasababu watu wanatumia nguvu nyingi zaidi kuliko maarifa, na wakati mwingine mabeki hawampi mtu hata nafasi ya kudhibiti mpira.

Hata hivyo amekiri kwamba hakuwa kwenye kiwango kizuri kutokana na kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu.

Akizungumza na gazeti hili Niang amesema, alikuwa kwenye mapumziko kwa muda mrefu kwahiyo ufiti wake umepungua kwa kiasi kikubwa na tangu amewasili Simba amefanya mazoezi kwa siku mbili na kikosi hicho.

“Nilihitaji nipewe muda zaidi wa kuzoeaa na wachezaji wa Simba, lakini pia kuzoea mfumo wa kocha na aina ya soka analotaka. Kwa bahati mbaya nimeonekana kama sijui mpira, lakini mimi ni straika mwenye heshima kubwa Senegal” amesema.

“Ni kweli sijaonesha kiwango kizuri kwasababu nimetoka likizo, na kila sehemu unapokwenda unahitaji muda ili kuzoea, mimi najaribu kuzoea mpira wa Simba. Sifahamiani na wachezaji, nimefanyanao mazoezi kwa siku mbili na tulikuwa na mechi kwahiyo nilikuwa najaribu kuendana na mfumo wao”, amesema Niang.

Akaongeza: “Kila mahali unapokwenda inabidi ujitahidi kuendana na aina ya soka lao, lakini niliamini kuwa kabla ya ligi kuanza ningekuwa nimezoea mazingira na ningeweza kuonesha ubora wangu”.

Hata hivyo amesema kwamba pamoja na kwamba ametupiwa virago, Simba wangemvumilia wangeweza kupata mambo makubwa kutoka kwake.

“Nilikuja nikiwa na uhakika kwamba kwa rekodi yangu ningesajiliwa. Sijui nini kimetokea, sijui utaratibu ambao unatumika Tanzania. Lakini ngoja watafute mtu mbadala kama wameona kwamba mimi sitawasaidia” amesema.

Funga kazi


WAKATI dirisha la usajili linafungwa rasmi Jumatatu ijayo, Simba imelazima kufunga usajili huo kwa kishindo.

Katika hatua unayoweza kuita ni “Funga Kazi”, Simba imelazimika kutumia tena fedha kumtumia tiketi ya ndege, straika wa kimataifa wa Senegal Pape Abdoulaye N'Daw mwenye umri wa miaka 21 ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Msenegali mwenzake Papa Niang ambaye alichemsha katika majaribio.

N’Daw hadi mapema wiki hii alikuwa anacheza katika timu ya Dinamo Bucuresti ya nchini Romania, lakini Simba haikulitazama hilo, ikamvuta kuja Msimbazi.

Kiongozi mmoja wa wekundu hao wa Msimbazi ameliambia MWANASOKA kwamba Simba imeachana na Msenegali, Papa Niang baada ya kumjaribu kwa dakika 45 tu jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Huu sasa ni usajili wa mwisho, tuna hakika kabisa kwamba Simba tutapata straika ambaye kocha wetu anamtaka. Shida sio kuwa na mshambuliaji tu, lakini kuwa na mshambuliaji ambaye ni wa kimataifa mwenye uwezo wa maana sana” amesema kiongozi huyo.

Licha ya Pape Abdoulaye N'Daw kinda mwenye umri wa miaka 21, Simba pia ilikuwa katika mikakati ya mwisho kumpata mshambuliaji mwingine wa kimataifa kutoka Mali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amekaririwa akisema Msenegali huyo na mchezaji mwingine kutoka Mali watafanyiwa majaribio na atakayevutia zaidi, ndiye atapewa mkataba.

Niang alikuja SImba SC baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga juu ya dau la usajili.

Niang kutoka klabu ya Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang jana alishindwa kabisa kuwashawishi wana Simba kwa soka yake.

Mchezaji huyo wa zamani wa CF Mounana ya Gabon, Al Shabab SC ya Kuwait, FC Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland alitarajiwa kuondoka kurejea kwao, ikiwa ni baada ya siku tatu za kuwa Dar es Salaam.

Awali Simba SC pi ilishindwa kumsajili mshambuliaji mwingine hatari wa Vital’O, Laudit Mavugo kufuatia klabu mbili za nchini humo kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 walizokubaliana awali.

Aidha, kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako kuliishitua Simba. Vital’O ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi kwenda klabu nyingine.

Julio aisifu Simba, lakini ajitabiria ubingwa


JAMHURI Kihwelo
KOCHA wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo amesema kwamba Simba ni timu nzuri, lakini akasema kwamba Mwadui ndiyo wataibuka mabingwa wa ligi kuu msimu ujao.

Kocha huyo ambaye aliwahi pia kuwa kocha wa Simba amesema kwamba jeuri hiyo inatokana na usajili, maandalizi na marekebisho madogo atakayoyafanya kwenye kikosi chake baada ya kubaini makosa machache kwenye kikosi hicho.

Julio alizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu kati ya Mwadui FC dhidi ya Simba SC kuelekea michuano ya ligi kuu Tanzania bara itakayoanza Septemba 12 mwaka huu.

“Kwanza nashukuru Mungu kucheza mechi ambayo ni kipimo kizuri kwangu maana nimeshacheza mechi na timu za Ligi Kuu takribani sita sasa na nimeona kadiri siku zinavyozidi kwenda wachezaji wangu wanabadilika ingawa leo nimecheza nikiwa na wachezaji saba wakiwa wako majeruruhi. Chuji anaumwa, Mnyati anaumwa, Antony Matogolo na wengine wengi”.

“Kwangu hiyo siyo ishu kwa maana nimesajili wachezaji kwa ajili ya Ligi kuu lakini uwezo wa ya timu yangu nimeifurahia kwa jinsi walivyocheza ingawa hatukupata goli”.

“Simba ni timu nzuri ila wao walichokosea ni kutudharau sisi na kuona sisi hatuna uwezo na wao kujiona timu yao inauwezo kuliko sisi. Hata kabla hatujacheza kuna baadhi ya wachezaji walisema, sisi tuna vijana wanapenya mtafungwa goli tano. Mimi nikawaambia uwezo wa kutufunga goli tano hamna twendeni tukacheze mpira”.

Julio akaendelea kwamba “Kingine naujua vizuri huu uwanja, walivyokuja walicheza kwa nguvu kwa presha ili kupata goli za mapema kwahiyo kadiri muda ulivyokuwa unakwenda halafu goli hawapati, morali ikawa imeshuka timu yangu ikatulia na kucheza vizuri ingawa hatukupata goli lakini performance mimi nimeifurahia hususan safu ya ulinzi na viungo wamecheza vizuri sana”.

Kocha huyo akasema tena “Mimi ndio nakuwa bingwa mwaka huu, nikisema hivyo watu wanacheka na kuniona mimi mwendawazimu. Lakini si mnajua kwamba sisi sote tutakufa? Lakini hatujui tutakufa lini kwahiyo kama wenzetu wametangulia wamekufa na sisi tutakufa kwahiyo hata mimi timu yangu inaweza kuwa bingwa. Tupo katika mashindano, basi nitajieni nyinyi timu itakayokuwa bingwa kwenye msimu huu tunaotarajia kuuanza mwezi Septemba”. “Kila timu ambayo imesajili, imejipanga, malengo yake ni kushinda kwahiyo na sisi tutapambana kwenye mbio ndefu halafu baadae ndio bingwa atapatikana lakini kwa timu yangu nilivyoiandaa na makosa ambayo nimeyaona nikiyafanyia marekebisho, kwa nini nisiwe bingwa?”.

Kerr: Mkinizingua naleta Wazungu


DYLAN Kerr
KOCHA Mkuu wa Simba, mwingereza Dylan Kerr amewachimba mkwara wachezaji wake, hasa wa safu ya ushambulizi akisema kwamba kuna siku atawafanyia kitu mbaya.

Kerr ameyasema hayo baada ya matokeo ya sare tasa kati ya Simba na Mwadui FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Jumatatu iliyopita.

Akiongea na MWANASOKA, kocha huyo mwenye msimamo mkali amesema kwamba hafurahishwi na safu ya ushambuliaji ya Simba inavyocheza.

“Niwe mkweli, sifurahishwi na mambo yanavyokwenda. Mimi ni kocha ninayetaka matokeo bora. Ninapoitazama safu yangu ya ushambuliaji natamani kusafiri kwenda Ulaya kusaka washambuliaji” amesema kocha huyo.

Alipoulizwa kwamba haoni kama washambuliaji wa Ulaya ni ghali sana kucheza Tanzania, alishangaa na kusema:

“Nani kakwambia kuna watu ghali Ulaya? Mimi nafahamu kuna watu watu wanaweza kuja kucheza hapa kwa mshahara huo huo wanaolipwa Waafrika. Tatizo muda wa kufanya hivyo kwasasa sina, Ligi inakaribia kuanza na usajili ndio huu mnaouona matokeo yake”.

Amesema kwamba katika bara la Ulaya na hata Amerika ya Kusini kuna baadhi ya wachezaji wazuri sana ambao hawapati nafasi katika nchi zao, na wangependa kucheza ili kulinda vipaji vyao na kuishi.

Ametoa mfano wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Countinho akisema kwamba katika nchi anakotoka ya Brazil kuna wachezaji wa maana sana ambao hawana nafasi kutoka na ushindani mkubwa wa soka la taifa hilo.

“Katika nchi kama Brazil anakotoka yule mchezaji wa Yanga, katika nchi kama Mexico na Uruguay kuna wachezaji ambao ukiwaleta hapa ni lulu kubwa” amesema.

Kocha huyo amesema jambo moja alilogundua ni kwamba wachezaji wengi wa Afrika hawajitumi ipasavyo, lakini akasema kwamba kama kocha anayafanyia kazi matatizo yaliyojitokeza katika kikosi chake kwa sasa.

Kauli hii ya Kerr inaleta tafsiri kwamba ikiwa wachezaji wa Simba hawataongeza bidii, kocha huyo anaweza kutumia nafasi ya usajili katika dirisha dogo kusajili wachezaji kutoka Ulaya wanaoweza kuisaidia Simba.

Ivo Mapunda: Sikuikacha Simba, nimeachwa


IVO Mapunda
KIPA aliyeisaidia sana Simba kupata walau mafanikio iliyoyapata kwenye msimu uliopita, Ivo Mapunda ameagana rasmi na Simba, lakini akasisitiza kwamba hajaikacha Simba kama inavyoripotiwa, ila Simba waliamua kumtema.

Mapunda, amesema anarejea Kenya, baada ya kuachwa na klabu hiyo mapema mwezi huu, na kwamba usahihi ni kwamba Simba imemuacha sio kweli kwamba hakuwa tayari kuidakia Simba kama inavyotangazwa.

Ivo aliyewahi kudakia pia Yanga SC, amesema hana kinyongo na Simba SC na anaondoka nafsi yake ikiwa safi kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.

“Nawashukuru mashabiki wa mpira haswa wa Simba kwa kuwa nami kipindi chote, nilipofanya vibaya na nilipowaudhi mlikuwa nami na ndiyo soka ipo hivyo,”amesema.

Ivo Ameongeza; “Maisha yana changamoto na ndiyo nimezipata kwa sasa Simba baada ya watu fulani kufanya hivyo, ila naamini maisha ni popote na Mungu ndiye kila kitu,”.

Ivo amesema kwamba anarudi Kenya ambako bado anakubalika na anaamini atapata timu.

Ivo alijiunga na Simba SC Desemba 2013 akitokea Gor Mahia ya Kenya katika cha mwaka mmoja na nusu wa klabu hiyo ya Msimbazi, ameidakia jumla ya mechi 39 na kufungwa mabao 25, akiiwezesha timu hiyo

Zaidi Ivo aliwafurahisha mno wana Simba kwa kulinda vyema lango kwenye mechi dhidi ya mahasimu, Yanga SC na kwa kipindi chake chote Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza mechi dhidi ya watani wao hao.

Alianza na mechi ya Nani Mtani Jembe mwaka juzi, Simba ikishinda 3-1, akadaka mechi ya Ligi Kuu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 kabla ya Desemba mwaka jana kuiongoza tena timu hiyo kushinda mechi ya Nani Jembe 2 mabao 2-0 na mechi yake ya mwisho ya watani kudaka, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 katika Ligi Kuu.

Kerr afumua kikosi cha Ligi Kuu


WAKATI ambapo Ligi Kuu ya msimu huu inatarajia kuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu, Kocha Mkuu wa Wekundu hao amepangua kikosi na kukipanga upya kwa mfumo wa 4:3:3 ambao umezaa matunda katika mechi za kirafiki.

Mfumo huo unatokana na matokeo ya mechi zote za kirafiki ambazo Simba imeshacheza, ambao kocha Kerr ameanza kupata mwelekeo wa kupata kikosi chake cha kwanza.

Ingawa ni mapema mno, lakini mwenendo mzima wa mazoezi ya hivi karibuni inaonesha namna mzungu huyo anavyoanza maandalizi ya kupata kikosi cha kwanza, huku akiwaamisha namba baadhi ya wanandinga wake.

Katika mazoezi ya jana na juzi katika uwanja wa Amaan, Unguja, Kerr ameanza kuwahamisha idara baadhi ya wachezaji, ikiwa ni baada ya kubaini majukumu yao dimbani.

Hatua ya awali ya kocha Kerr imeanza kwa kuangalia mfumo wa wachezaji wa idara ya ulinzi kwa kuwapanga Juuko Murshid acheze na Hassan Isihaka, Mohamed Hussein 'Tshabalala' Abdi Banda, hivyo ni sawa na kuwahakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

Katika idara ya kiungo, kocha huyo mzungu amewapa shavu kubwa Mwinyi Kazimoto, Justice Machabvi, Said Ndemla kuimarisha mfumo wa kuchezesha wachezaji watatu katika idara hiyo.

Mfumo wa kocha huyo umewapa nafasi wachezaji watatu katika safu ya kupanga mashambulizi kwa kuwapanga Peter Mwalyanzi, Mussa Hassan Mgosi na Ibrahim Ajibu na kuanzisha mfumo wa kuwa na washambuliaji watatu mbele.

Mfumo wa ambao kocha Kerr ameupanga ni kuchezesha mfumo wa 4:3:3 ambao umeanza kuzaa matunda katika mechi zote za kirafiki zilizochezwa na wanamsimbazi hao.

Kazi nyingine ilikuwa ni kupampanisha idara ya ulinzi na kiungo ambapo wachezaji Peter Mwalyanzi, Jonas Mkude,Said Ndemla, Simon Sserunkuma kwa mara nyingine wamepewa mbinu za kushuka hadi idara ya ulinzi na kupokea mipira na kupasiana haraka haraka huku wakikimbia kuelekea mbele.

Mfumo huu umewakosha makocha Dylan Kerr na Seleman Matola kwa wachezaji wote wa idara ya kiungo kuonyesha uwezo wa kucheza katika mfumo elekezi.

Akinukuliwa, kocha Kerr ameridhishwa na namna ambavyo mfumo wa 4:3:3 unavyoanza kuzoeleka na wachezaji, lakini akasisitiza kuwa fomesheni hiyo itategemea na aina ya timu npinzani watakayokutana nayo

"Tunaangalia uwezo wa kila mchezaji kabla ya kujenga kikosi.Tutaka kuona kila mchezaji anatekeleza jukumu lake na kutoa msaada kwa mwenzake wakati wote awapo mazoezini"

"Hii ndiyo ilikuwa kazi ya kipindi hiki cha mwisho cha kuandaa kikosi kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu" alisema Kerr.

Msenegal mpya aweka historia


Pape Abdoulaye N'Daw
KLABU ya soka ya Simba imeonesha jeuri moja kubwa. Imeachana na senegal Papa Niang. Lakini mara moja imemwita kundini msenegali mpya Pape Abdoulaye N'Daw.

N'Daw mwenye umri wa miaka 21, ametua jijini tayari kwa kuanza safari ya majaribio kabla ya kuliridhisha benchi la ufundi la kocha Dylan Kerr ambaye anahaha kupata mfumania nyavu wa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, straika huyo kinda ana histori ambayo kama itakwenda sawa na kiwango katika majaribio bila shaka itampa ulaji katika kikosi cha Simba cha msimu huu.

Msenegal huyo kwanza ana historia ya kufunga mabao kadri anapopangwa na alifanya hivyo akiwa katika FC Dinamo Bucuresti ya nchini Romania.

Akiwa na timu hiyo,N'Daw alipachika mabao saba katika mechi 11 alizopangwa, ikiwa ni wastani nzuri zaidi kuwekwa na wachezaji kinda wa mfano wake.

Lakini, hadi anavyotua jijini Dar es Salaam, msenegali huyo ameacha historia ya kuipachikia timu yake ya sasa ya Ligi Kuu ya Niary Tally ya nchini Senegal, straika huyo amepachika mabao matano katika mechi nane alizopangwa.

Kwa mujibu wa historia hii inamweka straika huyo katika nafasi kubwa ya kufuzu majaribio, kwasababu kitakwimu inaonesha kuwa anakidhi haja na vigezo vya mahitaji ya kocha Dylan Kerr.

Kocha Dylan Kerr amekuwa akiwahimiza viongozi wa klabu hiyo kupata straika wa maana wa kuiwezesha Simba kuwa na safu hatari ya kuipa ushindi timu katika mechi za Ligi Kuu inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi Septemba mwaka huu.

Awali,uongozi wa klabu ya Simba ilijipanga kumshusha kikosini straika Laudit Mavugo ambaye aliingia katika historia ya uwezo wa kupachika mabao katika ligi ya nchini Burundi, akiwa na timu yake ya Vital'0'.

Simba iliacha mpango wa kumwania Mavugo kutokana na dau ambalo Vital'0' ilikuwa ikihitaji la dola 11,000,000 ambalo sawa na shilingi 22 milioni, dau ambalo Wekundu wa Msimbazi waliona ni kubwa kwasababu awali hawakuambiwa kima hicho.

Kisha, Simba ilimgeukia mpachika mabao mwingine raia wa Burundi, Kelvin Ndayisenga ambaye hata hivyo kabla ya kuendelea na majaribio klabu yake na wakala walitaja dau la dola 70,000 ambalo ni sawa na takriban shilingi 140 milioni, hivyo wakaamua kuachana naye.

Simba yampata mrithi wa Mafisango


UKILITAJA jina la Patrick Mafisango katikati ya wanachama na washabiki wa klabu ya soka ya Simba, lazima watamkumbuka kwa simanzi! Kisha watakwambia 'Achana na ile Mashine, ni kiraka'.

Ukiwauliza sababu ya kuitwa 'kiraka' watakujibu, alikuwa na sifa ya kucheza kama, mlinzi, kiungo mkabaji na hata straika, wa kutuminiwa.

Huyu ndiye Mafisango (Patrick) ambaye amefariki dunia Mei 17 mwaka 2012 kwa ajali ya gari katika eneo la VETA, Chang'ombe, jijini Dar es Salaam, akiacha pengo kubwa la sifa ya mchango wale katika kikosi cha Msimbazi.

Lakini, kama ulikuwa katika mechi ya Simba dhidi ya Mwadui, kuna mchezaji mmoja anaitwa Justice Machabvi, huyu bwana achana naye, aliweka historia ya kucheza katika namba tatu tofauti dimbani kiasi cha kumshangaza Kocha Dylan Kerr na kulazimika kumvulia kofia na kumwita 'kiraka'.

Katika mechi ile iliyopigwa katika dimba la Taifa, Jumatatu iliyopita na Simba kutoshana nguvu na Mwadui kwa Suluhu, Machabvi, raia wa Zimbabwe alikuwa katika kiwango cha juu kiasi cha kumfanya Kerr azungumze ya mayoni.

Machabvi ambaye amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili, alianzishwa katika kikosi cha kwanza katika nafasi ya kiungo mkabaji na kuimarisha vyema ulinzi wa kikosi cha Wekundu hao.

Lakini, wakati ambapo timu ilipoendelea kupambana kwa ajili ya ushindi, Machabvi mara moja aliambiwa acheze kama kiungo wa kupandisha mashambulizi, kazi aliyoifanya na kumkuna kocha mzungu.

Wakati ambapo kocha Dylan Kerr alipobadilisha kikosi takriban kwa asilimia themanini, Justice Machabvi alipangwa kucheza katika nafasi ya ulinzi wa katikati, hasa baada ya kutolewa kwa 'mkoba' wa kutumainiwa, Juuko Murshid.

Katika kipindi hicho cha pili, Machabvi alionekana kumudu vyema nafasi ya beki wa kati kiasi cha kumfurahisha Dylan Kerr ambaye mara baada ya mchezo alimwagia sifa mzimbabwe huyo kwa kumwita 'kiraka'.

Kerr alimzungumzia Machabvi kama aina ya wachezaji anaotaka kuwa nao katika kikosi cha msimu huu kwa sababu wanabebwa na sifa ya kucheza katika namba zaidi ya tatu uwanjani.

"Machabvi ni aina ya wachezaji ninaowataka, alicheza vizuri na hata kuziba mapengo yaliyojitokeza wakati mchezo unaendelea".

"Ninahitaji wachezaji kama huyu, anayeweza kupewa jukumu na kulitekeleza vyema. Katika soka la zama hizi mchezaji lazima awe na uwezo wa kucheza zaidi ya namba mbili ama tatu". alisema Kerr.

Awali mara baada ya kutua kwa ajili ya kuinoa timu ya Simba, Kerr aliuambia uongozi azma yake ya kutaka kusajiliwa wachezaji walio na uwezo wa kucheza zaidi ya namba mbili dimbani.

Simba yashusha mtambo wa mabao

HAKUNA kulala hata kidogo Msimbazi! Simba imeamua kufanya kweli tena kwa kusaka mfumania nyavu ambapo jana imeshusha mtambo wa mabao kutoka nchini Mali.Huyu ni Makan Dembele.

Straika huyu mwenye umbile la maana amewasili nchini kwa majaribio chini ya kocha Dylan Kerr.

Kwa mujibu wa takwimu, Dembele ametua nchini akitokea katika klabu ya JS Kabylie ya Algeria.

Taarifa za ujio wa mpachika mabao huyo zinasema kuwa, mara baada ya kutua jijini Dembele anatarajia kuungana na kikosi cha Simba kinachokwenda kuweka kambi ya mazoezi kisiwani Unguja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Wekundu hao, Zacharia Hans Poppe alithibitisha kutua kwa mchezaji huyo na kwamba ni kati ya wachezaji wawili wanaokuja kufanya majaribio ya kuitumikia Simba ya msimu ujao wa ligi.

Hans Poppe alisema,awali kabla ya kuja nchini kamati yake ilikuwa na mawasiliano na wakala mbalimbali wa nchi za Afrika Magharibi na ndiyo waliosaidia kupatikana kwa Dembele na msenegal Pape Abdoulaye N'Daw aliyewasili kwa ajili ya majaribio.

"Ni kweli tumempokea Dembele na N'Daw ambao wamekuja kwa ajili ya majaribio kabla ya kufanyika kwa hatua nyingine za kiufundi na usajili utakaozingatia matakwa na maelezo ya benchi la ufundi". "Kocha Dylan Kerr ndiye aliyeachiwa jukumu la kuwaangaalia kiufundi kabla ya kutoa majibu ya mwisho ya kama wamefuzu au la" alisema Hans Poppe.

Monday, August 24, 2015

Twiga Stars mguu sawa kuwavaa Harambe Stars

TIMU ya taifa Tanzania katika soka la wanawake Twiga Stars, leo alhasiri inajitupa uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kupimana nguvu na wenzao wa Kenya, Harambee Starlets.

Wakenya hao waliowasili juzi asubuhi katika msafara wa watu 24, wamekuja kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki ambayo Twiga Stars wataitumia kama sehenu ya mazoezi kujiandaa na michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika mwezi ujao nchini Congo Brazaville.
Kikosi hicho kimekuja na wachezaji 17 na viongozi tisa.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), pambano hilo linalotarajiwa kuwa la kukata na shoka, litaanza saa 10:00 jioni.

Wakati walipowasili hapa nchini juzi, kocha mkuu wa timu hiyo David Ouma, alieleza kuvutiwa na hali ya utulivu, usalama wa Zanzibar pamoja na ukarimu wa wenyeji.

Hata hivyo, Ouma alisema pamoja na uhusiano wa miaka mingi kati ya nchi za Tanzania na Kenya, lakini wamekuja kushinda na hakuna mbadala wa lengo lao hilo.

“Nimekuja na visu vyangu vyote ambavyo ni vikali na nitavitumia bila huruma kumchinja Twiga keshokutwa (leo) katika uwanja wa Amaan,” alijigamba kocha huyo.

Amewataja baadhi ya wanasoka wake tegemeo kuwa ni Merik Nuzia, Tabaka Chacha, Mwanahalima Adam, Huendi Acheni na Dorias Chitobe.

Sophia Mwasikile ambae ni nahodha wa Twiga Stars, alisema timu yao iko imara kuwafundisha majirani zao hao jinsi ya kutumia nafasi za kufunga mabao na kwamba kazi ya kipa wao leo itakuwa kwenda kuokota mipira nyavuni mfululizo.

Hata hivyo, alitoa indhari kwamba lengo lao ni kuonesha kiwango kizuri na kwamba mchezo huo sio lengo kubwa kwao, bali wanachoangalia ni mashindano ya Afrika yaliyo mbele yao.