Wednesday, September 30, 2015

Zlatan Ibrahimovic adhihirisha ni mchezaji wa namna gani

psg
Zlatan Ibrahimovic ikifika November 25 atakua na mechi dhidi ya Malmo. Club hii ambayo ina makazi nchini Sweden ndio sehemu ambayo Zlatan amezaliwa na kuanza kucheza soka, kwa hiyo Zlatan atakua anarudi nyumbani kwao asili yake kabisa.
Zlatan haioni hiyo mechi kama sehemu ya mashindano lakini kwake ni sehemu ya furaha kwake kurudi nyumbani. Mechi hii itakua kwenye group A la Uefa Champions League. group hilo lina club kama Paris,Real Madrid,Shakhtar Donetsk na Malmo.
Hivi sasa Zlatan ameshakodi eneo kubwa la wazi ambalo lipo kwenye maeneo hayo ya Malmo na ataweka big screen na hakuna mtu atakae lipia kiingilio kuangalia mechi hiyo. Zlatan ametoa tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kwamba kuna suprise nyingi zinakuja.

No comments:

Post a Comment