Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu (TFF) Jamal Malinzi ameendelea kusisitiza kwamba Tanzania
itashiriki michuano ya kombe la dunia miaka ijayo kutokana na maandalizi
ambayo tayari yameanza kufanywa na shirikisho hilo kwa kuanza kujenga
timu za vijana.
Pia katika hilo Malinzi ameongeza
kwamba, tayari wameshaomba na kukubaliwa kuandaa michuano ya mataifa ya
Afrika kwa vijana wa U17 michuano inayotarajiwa kufanyika mwaka 2019
huku akisisitiza tayari timu kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo
imeshaanza kuanaliwa.
Malinzi ametoa kauli hiyo leo
wakati akifunga kozi ya makocha wa leseni C ya CAF iliyokuwa
ikifundishwa na Salum Madadi ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TFF.
“Sisi kama TFF tumesema kwamba
mwaka 2020 tutacheza fainali za Olympic za Tokyo tumesema hivyo na
tunaomba Mungu atusaidie”, amesema Malinzi.
“Kama tukiweza kufanikiwa 2020,
tukacheza fainali za Olympic Tokyo, 2026 tutakuwa na timu ya na timu ya
kucheza kombe la dunia mwaka 2026”.
No comments:
Post a Comment