Uongozi wa timu ya African Sports
‘wanakimanumanu’ umekiri kuwepo kwa hali ya sintofahamu baada ya
kukimbiwa na mchezaji wake Nsa Jobu aliyesajiliwa kukisaidia kikosi
hicho kilichopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Katibu mkuu wa kikosi hicho Khatibu Enzi amesema mchezaji huyo ametoweka kwenye kambi ya timu hiyo bila taarifa yoyote.
“Ni kweli Nsa Jobu mpaka dakika
hii taarifa zake zinakwenda tofauti kwa sababu mara ya kwanza tulipata
mawasasiliano kwamba amepatwa na msiba, lakini mpaka sasa mawasiliano
yanakwenda tofauti kwahiyo bado sijapata jibu la kuweza kumjibia”,
amesema Enzi.
“Kwa mara ya mwisho tumewasiliana
wiki moja iliyopita akatuelezea dharura zake na tukamfanikishia, lakini
kwa siku za hivi karibuni amekuwa hapatikani. Suala lake tumeliweka
pembeni kidogo sasahivi tunaangalia mambo ya mechi dhidi ya Mwadui”.
“Tuna mkatabanae wa mwaka mmoja,
hilo ni suala la klabu tunaweza kufanya marekebisho, kwasababu mikataba
ipo basi tutalifanyia kazi”.
Timu hizo zinakutana Septemba 17
(Alhamisi) kwenye mchezo wao wa raundi ya pili huku timu zote zikiwa
zimechezea vichapo kwenye mechi zao za kwanza, African Sports walibanwa
na Myama Simba kwenye uwanja wa Mkwakwani wakati Mwadui FC wao walikula
kibano kutoaka kwa Toto Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
No comments:
Post a Comment