Kivumbi
cha ligi kuu ya kandanda Tanzania bara kikiwa kimeanza, kikosi cha
maafande wa JKT Ruvu kimeshawasili jijini Mbeya tayari kwa mchezo wao wa
kuwania taji la ligi hiyo mchezo utakaopigwa siku ya Jumatano kwenye
uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Mtandao huu umezungumza na kocha
wa maafande hao Fred Felix Minziro kutaka kujua mikakati ya kikosi chake
kulekea mchezo huo mara baada ya kuchezea kichapo kwenye mchezo wa
kwanza mbele ya Majimaji ya Songea.
“Kwaujumla game haikuwa nzuri
kwetu na performance haikuwa kama tulivyotarajia kwahiyo ni vitu ambavyo
nimejaribu kuvifanyia masahihisho pamoja na mambo mengine madogomadogo
basi naamini Mungu akijalia mechi itakuwa nzuri Jumatano”, amesema
Minziro.
“Bado ninakikosi bora na imara na naamini nitafanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi”.
“Hakuna asiyejua kwamba Mbeya
City ni wazuri, mechi itakuwa ni yenye ushindani kutokana na Mbeya City
nao walivyofanya usajili na kuwa na kikosi imara”.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ni
moja kati ya mechi zitakazokuwa ngumu na ushindani mkubwa kutokana na
timu zote kupoteza mechi zao za kwanza msimu huu. Mbeya City wao
walipoteza mhezo wao wa kwanza wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani
mbele ya Kagera Sugar wakati JKT Ruvu wao walifungwa mchezo wao wa
kwanza na Majimaji ya Songea kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
No comments:
Post a Comment