Wednesday, September 9, 2015

Kumekucha Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu


RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

Septemba 12, 2015
Ndanda FC Vs Mgambo JKT
African Sports Vs Simba SC
Majimaji FC Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Prisons
Stand United Vs Mtibwa Sugar
Toto Africans Vs Mwadui
Mbeya City Vs Kagera Sugar
Septemba 13, 2015
Yanga SC Vs Coastal Union
Septemba 16, 2015
Yanga SC Vs Prisons
Mgambo JKT Vs Simba SC
Majimaji FC Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Azam FC
Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
Ndanda FC Vs Coastal Union
Septemba 17, 2015
Mwadui FC Vs African Sports
Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo JKT Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo JKT
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015
African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City
LIGIi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.
Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.
Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

No comments:

Post a Comment