Tuesday, September 1, 2015

Victor Moses asaini Chelsea apelekwa kwa mkopo West Ham


WINGA wa kimataifa wa Nigeria, Victor Moses amesaini Mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea Chelsea na kutolewa kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kwenda West Ham. 
Moses ambaye amekuwa jana nafasi tangu asajiliwe Stamford Bridge baada ya kucheza kwa mkopo msimu uliopita Stoke City na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo Liverpool.
Lakini winga huyo amesaini Mkataba mpya The Blues na sasa atakwedna kucheza tena kwa mkopo The Hammers kuendelea kukusanya uzoefu wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment