Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, kumeshuhudiwa tukio la kushangaza kwenye
soka la Tanzania baada ya timu ya KMC ya Kinondoni inayoshiriki ligi
daraja la kwanza (FDL) kufanya mabadiliko kwa kuwaingiza wachezaji wanne
kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu wa soka.
Tukio hilo lilitokea tarehe
27.9.2015 wakati KMC ikicheza dhidi ya Friends Rangers kwenye uwanja wa
Karume ambapo KMC ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Frank Mashoto
badala ya Kudra Omari, Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon, Mfanyeje
Musa badala ya Kabange Mgunda na Sultani Kasiras badala ya Adam Said.
Mechi hiyo namba 8 ya Kundi A ilimalizika kwa KMC kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Friends Rangers.
Baadae Friend Rangers ilikata
rufaa juu ya ushindi huo wa KMC kwasababu walikiuka kanuni na 14 (25) na
maamuzi yaliyotolewa na TFF tarehe 30.9.2015 yameipa ushindi timu ya
Friend Rangers huku KMC ikipigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa
akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa
onyo.
No comments:
Post a Comment