Wednesday, September 16, 2015

Copa Coca Cola kufanyika mwakani

MASHINDANO ya Copa Coca Cola yanayodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji
ya Coca Cola yaliyokuwa yafanyike katikati ya mwaka huu, sasa
yatafanyika mapema mwakani mwezi Februari kuanzia ngazi ya Wilaya na
fainali zake kufanyika mwezi Juni na Julai 2016.

Michuano hiyo ambayo hushirikisha timu za mikoa yote Tanzania kuanzia
katka ngazi ya Wilaya, hufanyika kila mwaka kwa kuwashirkisha vijana
wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Taarifa ya Idara ya Masoko ya Coca Cola imesema kampuni hiyo
imeahirisha kufanyika kwa michuano hiyo wa mwaka huu, na sasa itafanyika
mwakani ili waweze kupata nafasi ya kuandaa vizuri mashindano hayo.

Tuna uzoefu na mashindano hayo, ni vyema tukaifanya wakati wa likizo
wakati vijana wakiwa mapumziko, sababu wachezaji wote wa michuano ya
Copa Coca Cola ni wanafunzi hivyo ni vizuri tukaandaa mashindano hayo
wakati wanafunzi wakiwa likizo.

Michuano ya Copa Coca Cola ilianza mwaka 2007 kwa kushirikisha vijana
wenye umri chini ya miaka 17 (U17) na baadae mwaka 2012 kubadilishwa na
kuwa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Baadhi ya wachezaji waliopatikana katika mashindano hayo kwa sasa
wanacheza katika vilabu vikubwa vya Ligi Kuu ya Vodacom nchini na
wengine wamepata naafasi ya kucheza soka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment