David
de Gea ameachwa njia panda asubuhi ya leo baada ya kusubiri kwa muda
mrefu kuhama kutoka Manchester United kwenda Real Madrid kufuatia baadhi
ya ‘documents’ kushindwa kufika kwenye makao makuu ya bodi ya usajili
ya Hispania wakati vilabu hivyo vikijaribu kufanya uhamisho wa mlinda
mlango huyo usiku wa manane hadi dirisha la usajili kufungwa nchini
Hispania.
De Gea alikuwa akiamni kwamba,
ndoto zake zimetimia za kuhamia Madrid kufuatia miamba hiyo ya La Liga
kuvunja ukimya na kuikatia Man U kitita cha pauni milioni 29 jana
(Jumatatu) mchana. Golikipa wa Madrid Keylor Navas pia alikuwa sehemu ya
dili hilo ambapo angejiunga na Manchester kama sehemu ya usajilin wa De
Gea.
Chanzo kutoka Real Madri
kinasema kwamba, Madrid wanailaumu Manchester United kwa kushindwa
kutuma doments sahihi kwenda LFP shirikisho la soka la Hispania jana
usiku.United wamekanusha madai hayo
wakisema kuwa, walipata uhakika kuwa document zao zimetumwa kwa wakati
muafaka unaotambuliwa na FIFA. Uongozi wa LFP unasema United walizijaza document hizo kwa mfumo ambao mtu mwingine asingeweza kuzifungua.
Klabu zote zinataka dili hilo likamilishwe na zinatarajia leo (Jumanne) kukata rufaa kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.
No comments:
Post a Comment