Wachezaji wengi wa ngazi za juu
wa Kiafrika wanaochezea ligi kuu Uingereza inasemekana wanaamini sana
katika nguvu za giza kupata mafanikio katika soka.
Ripoti kutoka gazeti la the Sun
zinadai kwamba wachezaji hao nyota wanaoamini katika hilo hutumia maelfu
ya pauni kuwapa waganga wa kienyeji ili kuwapandisha viwango vyao.
Wachezaji hao huenda kwa wapiga
juju huko Afrika Magharibi, ambapo huoneshwa namna ya kufanya mambo ya
miujiza ambayo pia husemekana kuondoa mikosi hasa ya majeraha ya mara
kwa mara kwa wachezaji hao.
Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu
mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor alimshuku mama yake kutumia
nguvu za uchawi kumroga ili asiweze kupacika mabao pindi awapo uwanjani.
Hata hivyo, mshambuliaji wa zamani wa West Brom Brown Ideye amewaonya baadhi ya mastaa hao kwa kuamini katika nguvu hizo.
Ideye alisema: “Nafahamu baadhi
ya wachezaji ambao hutumia nguvu hizo lakini hawafanikiwi. Huu ni upuuzi
tu. Wanaweza kupata mafanikio ya muda mfupi, lakini huwagharimu katika
kipindi kirefu cha maisha yao. Waganga wana ushawishi mkubwa sana.
“Mara zote hawa ni watu ambao hujitahidi kujitafutia utajiri kwa njia zisizo halali kwa kukuambia uongo.
“Kama mambo kama haya yangekuwa
yanafanyika, basi leo hii badala ya Messi na Ronaldo kuwa wanashinda
kila siku uchezaji bora wa dunia, ingekuwa ni kwa wachezaji wa Kiafrika.
Baadhi ya uchawi hugharimu mpa Yuro 460 kwa mara moja.
No comments:
Post a Comment