Shirikisho la Soka nchini (TFF) limepitisha malipo ya Sh. 350,000 kwa kila mwamuzi wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.
Mtandao huu umebaini kuwa Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Zanzibar Juni 20 mwaka huu, ilipitisha kanuni mpya za ligi msimu huu huku ikiongeza fungu bla malipo kwa marefa.
Kanuni mpya Na. 26 (3) na vifungu vyake (c) na (d) vinasema: “Mwamuzi sasa atalipwa Sh. 200,000, posho ya kujikimu na usafiri wa ndani Sh. 150,000 na nauli kutoka mkoa husika kwenda kituo cha mechi na kurudi alikotoka.”
Usafiri ulioidhinishwa na shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini ni mabasi, meli au treni daraja la pili.
No comments:
Post a Comment