Mlinzi wa Arsenal Gabriel ameshinda rufaa yake baada ya klabu yake kupeleka ushahidi wa picha za video kumtetea mlinzi huyo.
Mwamuzi Mike Dean aliyechezesha
mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita, alimtoa nje
kwa kadi nyekundu beki huyo raia wa Brazil akidaiwa kumganyaga kwa nyuma
mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa lakini picha za video zilizopelekwa
kama ushahidi kwenye chama cha soka cha England (FA) hazioneshi kama
Costa aliguswa na mguu wa Gabriel.
Chama cha soka nchini England
kiliendelea kusubiri hadi saa 12 jioni siku ya Jumanne kuona kama Costa
atawasilisha rufaa yake lakini haikuwa hivyo na kupitisha adhabu ya
kumfungia mechi tatu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
tayari ameshaamua kumtumia Radamel Falcao kwenye mechi dhidi ya Walsall
siku ya Jumatano kwenye mchezo wa kombe la Capital One.
Lakini wakati huohuo, Gabriel
bado anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu aliounesha mara baada ya
kuoneshwa kadi nyekundu na Mike Dean huku akionekana kutaka kugoma
kutoka nje ya uwanja.
Lakini maamuzi hayo yanamaanisha Gabriel atacheza mchezo wa Capita One siku ya Jumatano dhidi ya Tottenham.
No comments:
Post a Comment