Nidhamu ni kitu cha msingi sana kwenye kazi yoyote zaidi ya uwezo wako ulionao kwenye kufanya hiyo kazi. Vidal hivi sasa kafukuzwa na kocha wake Jorge Sampaoli arudi kupumzika hadi atakapo kuwa fit.
Chile ipo kwenye mazoezi ikitegemea kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Paraguay. Wachezaji wapo pamoja kwa ajili ya mazoezi lakini Vidal aliripoti kwenye kambi ya timu ya taifa Jumanne mchana akiwa bado ana pombe kichwani mwake. Kocha Sampaoli alimrudisha na kumwambia arudi Ujerumani hadi pale atakapo kuwa tayari. Kocha huyo pia alimpa onyo kali mchezaji huyo kwamba anampa nafasi ya mwisho.
Vidal aliwai kuhatarisha maisha yake na ya mpenzi wake baada ya kupata ajali ya Ferrari baada ya kunywa pombe usiku mkali huko Santiago. Baada ya kuomba msamaha kwa machozi akaruhusiwa kujiunga tena na Chile na kushinda Copa America.
Chama cha soka cha Chile kimetoa statement kwamba Vidal karudishwa ujerumani kwasababu ya matatizo yake binafsi.
No comments:
Post a Comment