Aliwai kupewa jina la Ade Mabao na baadhi ya mashabiki wa soka hapa bongo lakini mambo yake kwenye kazi hiyo kwa sasa hayaendi vizuri. Siku za mwisho za kufanya usajili Adebayor alitakiwa kuhamia club ya West Ham lakini pia Hammers walisema kwamba gharama ya mchezaji huyo ni kubwa sana.
Sasa hivi Spurs wanakaribia kutoa kikosi chao kamili cha wachezaji 25 kwenye EPL na Adebayor inaripotiwa atakatwa kutoka kutoka kwenye hicho kikosi.
Manager Mauricio Pochettino alimtoa Adebayor kwenye kikosi cha kwanza tangu miezi 12 iliyopita. Kutokana na mchezaji huyo kushindwa kukamilisha uhamisho wa kuhama club hiyo, ataendelea kuwepo Spurs lakini hatocheza. Adebayor kwa sasa analipwa £100,000, lakini hakuna dili lilifanikiwa kumhamisha kutoka Spurs hadi deadline inafika.
No comments:
Post a Comment