Mshambuliajin wa Manchester Unitd,
Javier Hernandez ‘Chicharito’ amehamia ligi ya Bundesliga kunako klabu
ya Bayer Leverkusen kwa dau la pauni milioni 12.
Chicharito ametua Ujerumani jana
asubuhi akiwa ameruhusiwa kuondoka Old Trafford majira haya ya joto
baada ya kushindwa kumshawishi kocha wa timu hiyo Lois van Gaal.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27
msimu uliopita aliutumia akiwa kwenye ligi ya La Liga akikipiga kwa
miamba ya Hispania timu ya Real Madrid. Japo United inauhaba wa
washambuliaji Chicharito bado hakuweza kupata nafasi kwenye kikosi hicho
wakati timu yake ya zamani ikiangukia pua mbele ya Swansea Jumapili
iliopita.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa
Mexico amesaini mkataba wa miaka mitatu baada ya pande zote mbili
kukubaliana ada ya pauni milioni 12.
West Ham walikuwa wakivutiwa na
Chicharito na walikuwa tayari kumsainisha mkataba lakini walishindwa
kufanya hivyo kutokana na mchezaji huyo kuhitaji mshahara ambao West Ham
waliona hawawezi kumudu kumlipa.
No comments:
Post a Comment