MSHAMBULIAJI wa Juventus, Alvaro Morata amekanusha uvumi
ulioneea kwamba anaweza kurudi Real Madrid wakati wa majira ya joto yajayo
baada ya kubainisha kuwa kwa sasa amejikita katika klabu yake ya sasa.
Morata aliondoka Madrid na kujiunga Juventus msimu uliopita,
lakini Klabu hiyo ya Hispania imesema
inaweza kumsajili mchezaji huyo kwa ada inayotajwa kuwa ni euro milioni 25
mwishoni mwa msimu wa 2015-16.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Hispania,
ambaye amefunga magoli 15 katika mashindano yote kwa Juve msimu uliopita na
kuuiwezesha kushinda taji lake la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Italia, Scudetto
na kufika fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya, amesisitiza anafuraha kubakia Turin.
“Hakuna jinsi, Juventus ni timu yangu niko safi hapa,” alisema
Morata wakati alipoulizwa na gazeti la Sport Mediaset kama anashauku ya kurudi
Real.
“Sifikirii kuhusu kuondoka katika Klabu hii.”
Morata aliongeza katika mahojiano na Sky Sports Italia:
“Nakubali kwamba, Madrid wanahitaji mimi, lakini kwa sasa akili yangu ni
kufunga na kushinda kila kitu kinachowezekana nikiwa na Juventus.”
Juve ambayo imeaanza Ligi Kuu ya Italia, Serie A, bila ushindi
katika mechi tatu lao Jumapili itacheza na Genoa.
No comments:
Post a Comment