Mshambuliaji wa Chelsea Diego
Costa anaweza kupewa adhabu ya hadi mechi tatu na chama cha soka nchini
England baada ya mchezo usio wa kiuungwana kwa mlinzi wa Arsenal Laurent
Koscienly katika mchezo wa jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo uliomalizika
kwa Chelsea kushinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, ulimalizika kwa Arsenal
kuwa na wachezaji wawili pungufu waliooneshwa kadi nyekundu na mwamuzi
Mike Dean.
Costa ambaye anakabiliwa na
adhabu kwa mchezo mbaya kwa Koscienly alioneshwa kadi ya njano na
mwamuzi Mike Dean ambaye hata hivyo haikujulikana kadi hiyo ni kwa kosa
la Koscienly au ni majibizano yake na Gabriel Paulista ambaye pia
alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuingia katika mtego wa Costa.
FA
waliipitia ripoti yenye utata ya mwamuzi Mike Dean ambaye hakumuadhibu
Diego Costa kwa kitendo hicho kwa madai ya kutoona uzuri kilichotokea.
FA pia wamempa adhabu Gabriel
Paulista kwa kitendo chake kilichopelekea kupigwa kadi nyekundu, wakati
Saint Carzola akipewa onyo kali, na klabu zote mbili za Arsenal na
Chelsea zikipigwa faini kwa kutowafunza adabu wachezaji wake. Wote
wamepewa hadi saa kumi na mbili jioni jumanne hii kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment